Pilipili manga ni kiungo maarufu kinachojulikana pia kama mfalme wa viungo. Kupanda pilipili manga kuna umuhimu mzuri wa kiuchumi kutokana na mapato.
Aina zilizoboreshwa za kibiashara za pilipili manga nchini India ni Panniyur 1; hutoa mavuno takriban 1240 kg kwa kila hektari. Panniyur 2; hutoa mavuno takriban 2600kg kwa kila hektari, Panniyur 3; hutoa mavuno takriban 1950 kg kwa kila hektari, Panniyur 4; hutoa mavuno takriban 1270 kg kwa kila hektari, panniyur 5; hutoa mavuno takriban 1100 kg kwa kila hektari. Subhakara; hutoa mavuno takriban 2350 kg kwa kila hektari, Sreekara; hutoa mavuno takriban 2680 kg kwa kila hektari, Panchami; hutoa mavuno takriban 2800 kg kwa kila hektari, na Pournami ambayo hutoa takriban 2300 kg kwa kila hektari.
Mahitaji ya udongo na hali ya hewa
Pilipili manga hustawi vyema katika maeneo ya kitropiki, yenye joto na unyevunyevu, na mvua ya kila mwaka ya takriban sm 200. Udongo unaofaa kwa kupanda pilipili manga unapaswa kuwa udongo mwekundu na tifutifu, wenye mboji, usio na maji mengi sana, na wenye pH ya 5 hadi 6.5.
Pilipili manga huenezwa na vipandikizi au mbegu. Hata hivyo, mbegu huchukua muda mrefu kukua na hazifai kwa kilimo cha kibiashara. Hata hivyo, panda vipandikizi vya pilipili manga vilivyo na vijicho 2–3 kwenye vikapu vya mianzi vilivyojazwa udongo, au tumia viriba vya plastiki.
Kupanda pilipili manga
Vipandikizi vya pilipili manga huwa tayari kupandikizwa ndani ya miezi 3. Walakini, pilipili manga huhitaji vijiti ili kuimarishwa kwani ni mimea inayotambaa. Panda pilipili manga kwa umbali wa mita 3–4, kwa upana wa mita 0.5 kwa 0.5 na kwa umbali. Acha umbali wa cm 30 kutoka kwa kijiti kinachoimarisha mmea.
Kabla msimu wa mvua hujaanza, panda vipandikizi vyenye mizizi 2–3 kwenye mashimo yaliyojazwa udongo na samadi iliyooza. Angalau kijicho kimoja cha kipandikizi kinapaswa kuingia udongoni, na vingine vibaki juu ya ardhi.
Palilia shamba ili kupata mavuno bora, ukuaji bora na uingizaji mzuri wa hewa. Ondoa machipukizi yoyote ya ziada.
Uvunaji wa pilipili manga
Pilipili manga huwa tayari kuvunwa wakati matunda yanapoanza kuonyesha rangi nyekundu, yaanimiezi 6–7 baada ya kupandwa. Vuna pilipili manga kwa mikono na kisha ikaushie juani.
Wadudu na magonjwa wakuu wa pilipili manga ni mende, wadudu wadogo, utiriri, na mnyauko.