Mitende huhitaji joto la juu sana hasa wakati wa kukomaa kama ilivyo katika Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati. Mitende pia huhitaji maji hasa wakati wa ukuaji wa mimea. Umwagiliaji wa mitende unaweza kuwa wa mafuriko au umwagiliaji kwa njia ya matone, lakini umwagiliaji kwa njia ya matone unapendekezwa kwa kuwa husababisha ufanisi mkubwa wa matumizi ya maji.
Mazoea ya usimamizi
Ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya maji, unaweza kuwa na kipima unyevu ardhini ili kupima kiwango cha unyevu kilicho kwenye udongo, na kumsaidia mkulima kurekebisha ratiba ya umwagiliaji ipasavyo.
Ili kuongeza ubora na ukubwa wa tende, unaweza kupunguza idadi ya tende zilizo kwenye kishada katika hatua ya awali ya ukuaji. Hivyo tende zilizosalia zinaweza kukua zaidi bila kukwaruzana kwa hivyo ziwe za ubora wa juu.
Tende zinaweza kupandwa kiasili bila kutumia dawa za kuulia wadudu na mbolea za madini.