Bila usimamizi mzuri, mazao ya minanasi hushuka sana baada ya mavuno ya pili. Katika video hii tunaangalia jinsi ya kudumisha uzalishaji wa shamba kwa angalau miaka 6.
Minanasi hukua vizuri kwenye udongo iloyokauka vizuri na wenye rutuba. Mboji inaweza kutoka kwa makapi ya kahawa na samadi ya kuku. Makapi ya kahawa hutoa virutubisho polepole lakini kwa muda mrefu kuliko samadi ya kuku. Baada ya kuongeza samadi, Fanya miinuko ya udongo kwenye safu za minanasi, lakini usitumie samadi ya kuku kama unakuza kwa ajili ya soko la mazao asili. Unaweza kupanda mimea mingine ya jamii ya kunde kati ya safu, kwa sababu huongeza rutuba ya udongo, hutoa chakula, huandamiza magugu na hufanya kama chanzo cha mapato kabla ya mavuno ya mananasi. Baada ya mavuno, tumia mabaki ya mazao kama matandazo, na wakati wa kukodisha ardhi anzisha mikataba ya ukodeshaji wa ardhi.
Njia bora ya kilimo mseto cha mananasi
Panda minanasi bila kufuata muinamo wa shamba kati ya safu mbili, ukiacha nafasi ya cm 30–50 katikati. Acha nafasi ya mita 1 hadi 1.5 kati ya kila safu mbili, na panda mazao ya mikunde katika nafasi pana.
Baada ya miezi 3 weka mbolea ya samadi, mbolea oza au mapaki ya kahawa kati ya mimea ya minanasi. Fanya miinuko ya udongo kwenye safu za minanasi na uwape kivuli kwa kukuza migomba au miti ya mkunde kwa nafasi pana, ambayo pia huongeza nitrojeni kwenye udongo. Punguza mimea yote ya vivuli mara kwa mara ili kuepuka kivuli kingi sana.