Kukuza vitunguu kutoka kwa mbegu kunahitaji uangalifu mkubwa. Baada ya mbegu kuota, miche michanga inapaswa kulindwa kutokana na jua kali na mvua nyingi.
Kitalu cha mbegu hukuruhusu kumwagilia maji kwa urahisi na kulinda miche yako ya vitunguu hadi iwe na nguvu ya kutosha kupandikiza shambani. Kuanzisha kitalu hukuwezesha kutunza vyema miche yako ya vitunguu. Mche wa vitunguu unahitaji udongo tifutifu wenye afya. Kitalu cha mbegu kitahitajika kuinuliwa wakati wa mvua ili mizizi ya vitunguu isioze. Mbolea iliyooza vizuri au mboji huongezwa kwenye udongo wakati wa kupanda miche ya vitunguu.
Kupanda mbegu
Kutumia mbegu bora huhakikisha kwamba mbegu nyingi huota. Miche ya vitunguu huhitaji nafasi ya kutosha ili istawi vyema. Panda mbegu kwenye safu kwa umbali wa sm 5-10 na zipandwe kwenye mashimo ya kina cha sentimita 1 na kisha zifunikwe na udongo laini.
Ongeza matandazo na uyaondoe mara tu miche inapotokea. Kumwagilia kitalu hufanyika asubuhi na mapema na huku husababisha miche yenye afya ambayo ni muhimu kwa mavuno mazuri.