Vitunguu vina mizizi dhaifu, ya kina kifupi. Shamba la vitunguu huhitaji udongo laini au tifutifu wenye rutuba katika wakati wa msimu wa kiangazi na mvua. Ili kupata mavuno zaidi, vitunguu huhitaji maandalizi bora ya shamba, na utunzaji bora wa miche.
Kwa mavuno bora, unafaa kuchagua shamba linalofaa, kuandaa vitalu na kupandikiza miche kwa njia bora.
Maandalizi ya shamba
Chagua shamba lenye rutuba ambapo vitunguu havijapandwa kwa muda wa miaka 3. Walakini, epuka kupanda vitunguu katika udongo wenye mchanga sana na udongo wa mfinyanzi. Kwaani aina hizo za udongo hazina rutuba ya kutosha na hukauka haraka. Mwishowe usipande vitunguu katika nyanda za chini zilizo na udongo wa mfinyanzi wakati wa msimu wa mvua ili kuepusha kuoza kwa mizizi. Mwagilia maji shamba wakati mvua ni chache kupoza joto la udongo. Inua kitalu cha mmea na kiwe na upana wa mita 1 ili kuweka mtiririko mzuri wa maji na kwa kurahisisha kuvifanyia kazi. Kwa kuongezea, lainisha udongo na ongeza mbolea au mboji kwa ukuaji wa mizizi. Tandaza na kusawazisha shamba ili kuwezesha mzizi mustawi.
Kutunza miche
Punguza kiasi cha maji unachomwagilia kabla ya kupandikiza ili kuongeza nguvu ya mimea. Mwagilia mimea maji na tumia zana sahihi wakati wa kupandikiza ili kuepusha mizizi kuharibika. Safirisha miche kwenye gunia lenye majimaji ili kuhakikisha hainyauki. Chimba shimo la kina cha nusu ya kidole ardhini na uache nafasi sahihi kisha upande mche mmoja ili jani na mzizi iweze kumea.
Mwagilia vitunguu maji baada ya kupandikiza ili kudhibiti miche dhidi ya kunyauka. Palilia shamba na ongeza mbolea kati ya mistari ya mimea kudhibiti ushindani na kuongeza rutuba ya udongo. Ongeza mbolea ya kikaboni ili kuboresha afya ya udongo.