»Kuchunguza kuepo kwa vuwavijeshi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/node/10689

Muda: 

00:14:10
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

Agro-Insight and FAO

Ikiwa unajua kutambua na kutoa viwavijeshi, basi ni rahisi kuwadhibiti.

Viwavijeshi, mara nyingi hujeficha ndani kabisa ya shina la mahindi ambapo dawa haziwezi kuwafikia na kuwaua. Kwa hivyo, lazima wakulima wawatafute na kuwaua ili waweze kupata mavuno. Viwavijeshi hupenda kula majani ya mahindi, lakini pia wanaweza kuishi katika mimea mingine. Wanaanza na kula madirisha madogo kwenye majani, amabao huendelea kugeuka matundu makubwa.

Maisha ya nondo

Nondo wa viwavijeshi anaweza kupaa umbali mrefu , na pia hutaga hadi mayai 200 kwenye jani moja. Unaweza kutambua mkusanyiko wa mayai ya nondo ambao kwamba waweza kuwa na ukubwa uliolingana na kidole kigumba na hufunikwa na manyoya laini meupe.

Siku 3 baada ya kutaga, viwavijeshi wadogo huanguliwa kutoka kwenye mayai, wanakwaruza majani wakitambaa na hivyo huacha madirisha madogo kwa majani. Na kwa siku 3 zijazo, huwa wanatafuata shina la majani kujificha. Katika wakati huu, madirisa hugeuka matundu makubwa kwasababu viwavijesha huwa wamekua wanono. Ukifunua shina la majani , unaweza kumpata kiwavijeshi kimoja tu, kwasababu huwa wanawala wenzao ili kupunguza kushindania chakula.

Baada ya wakati wawiki 2-3 , viwavijeshi huondoka huanguka kwa ardhi. Kisha wakichimba umbali usiozidi urefu wa kidole ardhini, ambapo hujifunika kwa kifukofuko cha rangi ya hudhurungi.

Wiki mbili baada ya hapo, nondo mzima hutoka kwenye hiki kifukofuko, hupaa na huanza kutaga mayai mapya,

kuua viwavijeshi kwa mkono

Tembelea shambani lako kila asubuhi baada ya siku 3 katika wiki 6 za kwanza, na ukague kama kuna ishaara zozote za shambulio la wadudu. Unapoona kinyesi cha mayai, basi kunjia mayai haya kwenya majani na kuwavunja na mkono wako.

Unaweza pia kueka kijiko kimoja cha udongo, jivu au mchanga kwenye china la mmea ili kuua viwavijeshi.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:45Viwavijeshi walitoka America kwa Africa mwaka wa 2016.
01:4602:51Viuatilifu / dawa za wadudu huwa bei kali, na huhatarisha maisha, na pia hushindwa kuua viwavijeshi wote walio shambani.
02:5203:55Viwavijeshi wanaweza kuishi katika mimea mingine, lakini wanapenda sana majani ya mahindi.
03:5604:14Viwavijeshi hutoka kwenye mayai yalio tagwa na nondo.
04:1504:32mkusanyiko wa mayai ya nondo ambao kwamba waweza kuwa na ukubwa uliolingana na kidole kigumba na hufunikwa na manyoya laini meupe.
04:3204:59Siku tatu baada ya kutaga mayai, viwavijeshi hutoka
05:0005:25Katika mda wa siku tano baada ya kutotolewa katika mayai, viwavijeshi hutafuta shina la majani kujificha
05:2605:40Mvua ikinyesha kabisa, viwavijeshi huanguka chini na hufa.
05:4106:15Viwavijeshi huwa na alaama ya herufi ya “ Y“ amabayo imepinduka juu chini kwa vichwa vyao.
06:1606:45Baada ya wakati wawiki 2-3 , viwavijeshi huondoka na huanguka kwa ardhi na hujifunika kwa kifukofuko cha rangi ya hudhurungi.
06:4606:53Wiki mbili baada ya hapo, nondo mzima hutoka kwenye hiki kifukofuko, huanza kutaga mayai mapya.
06:5407:11Mimea mingi huvumia Uharibifu wa majani.
07:1207:42Viwavi huharibu mahindi kiasi kidogo yakianza kukauka.
07:4308:58Tembelea na ukague shamba lako kila mara, kuwaua mayai kwa kutumia mkono.
08:5910:05Tembelea shamba lako mara mbili kwa wiki katika wiki sita za kwanza.
10:0610:57Unaweza pia kueka udongo kiasi, jivu au mchanga kwenye china la mmea ili kuua viwavijeshi.
10:5812:11Waweza pia kupata msaada kutoka kwa watoa huduma wa shamba.
12:1214:10muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *