Maembe ni matunda yaliyo na ladha nzuri lakini huathiriwa sana na wadudu kama vile dumuzi wa mbegu. Udhibiti wa mara kwa mara huboresha uzalishaji wa embe.
Dumuzi wa mbegu ya embe huharibu nyama na mbegu, na hivyo kusababisha matunda kuanguka mapema kabla ya kukomaa. Maisha ya dumuzi wa mbegu ya embe: Dumuzi waliyokomaa huwa kati ya rangi ya hudhurungi hadi kijivu kilichokolea. Rangi hii huwawezesha kuishi kwenye kokwa la mti wakati wa msimu wa matunda. Dumuzi hula maembe pekee, na wanaweza kuishi kwa muda mrefu bila kula. Dumuzi wazima huelekea kwenye matawi ili kuzaliana na kisha hutaga mayai ambayo huanguliwa na kuwa mabuu baada ya siku 3–4. Mabuu hupenyeza kwenye mbegu ambapo wataendelea kula mpaka wawe dumuzi wazima. Dumuzi wazima huacha mbegu na kuelekea na kujificha kwenye maganda ya mti, matawi au majani yaliyoanguka.
Mitego ya dumuzi
Daima, kuwa mwangalifu ili kutambua wadudu walioko kwenye bustani ya matunda, na kutumia utepe wenye gundi ambao hutega na kunasa dumuzi. Pia nyunyiza dawa za kuua wadudu. Hata hivyo, dawa hizi ni ghali na zina madhara kwa afya ya watu, mazingira na kuua wadudu marafiki shambani. Himizisha koyokoyo shambani ili waweze kula dumuzi. Choma mbangimwitu, pamoja na majani ya tithonia ili kutoa moshi ambao hufukuza dumuzi.
Zingatia mbinu bora za kilimo kama vile kuharibu matunda yaliyodondoka, kuzika matunda yaliyoanguka katika shimo la angalau 50cm ili kuua dumuzi wanaotokea. Mwishowe, kusanya na haribu matunda yaliyoanguka angalau mara moja kwa wiki. Pogoa miti ili kupunguza mazingira yenye unyevu ambayo hupendwa na dumuzi.