Ngano na shayiri ni miongoni mwa mazao muhimu ya nafaka duniani isipokuwa mpunga na mahindi, walakini huathiriwa na magonjwa ya kutu ambayo hupungua mavuno.
Udhibiti wa ugonjwa ni kwa kutumia aina sugu za mimea. Hizi hustahimili na kupunguza mashambulizi ya magonjwa ya kutu. Kutibu mbegu huzilinda dhidi ya magonjwa ya kutu na ni muhimu kukuza mazao yenye afya. Unaweza kupaka mbegu zako na mkojo wa ng’ombe na kinyesi. Ili kupaka kilo 1 ya mbegu, changanya glasi nusu ya mkojo wa ng’ombe na kikombe 1 cha samadi mbichi ya ng’ombe na uweke mbegu kwenye tope kisha kausha mbegu zilizopakwa kwenye kivuli kabla ya kupanda. Mbegu pia zinaweza kupakwa dawa ya trichodema.
Udhibiti wa shambani
Daima chunguza na ufuatilie uwepo wa ugonjwa hasa wakati hali ya unyevu na mvua. Katika shamba, unaweza kunyunyiza mchanganyiko wa trichodema wiki 3 baada ya kupandikiza.
Unaweza kutengeneza dawa yako ya kikaboni kwa kuchanganya konzi moja ya kinyesi cha ng’ombe, nusu lita ya mkojo na konzi 2 za majani ya mwarobaini katika lita 10 za maji. Weka mchanganyiko kwenye kivuli kwa siku 2 na kisha uuchuje. Kwa nusu hekta, changanya mchanganyiko uliyochujwa katika lita 250 za maji na nyunyizia asubuhi au jioni.
Iwapo yote hapo juu hayatafaulu, nyunyizia maziwa ya siagi ambayo yamechacha kwa kwa siku 10 hadi 15. Kwa nusu hekta, changanya lita 7 za maziwa haya katika lita 250 za maji na unyunyizie.
Unaweza pia kuchanganya nusu kikombe cha unga wa majani makavu ya amaranthus nyekundu, mnanaa au hibiscus, na kuyachanganya katika lita 250 za maji. Weka mchanganyiko usiku kucha na uchuje ili kunyunyizia mazao siku inayofuata na tena baada ya siku 15.