Endapo unaishi katika eneo lenye mvua kidogo, unaweza kuongeza uwezekano wa kuvuna mazao mengi kwa kuhakikisha unaendana na msimu wa mvua, na mazao yamerutubishwa vyema.
Lima shamba kabla ya mvua kuanza, kwa kina kirefu na pande kwenye mistari, kwa sababu kufanya huku kunasaidia kuvunjavunja udongo ulioganda na kuruhusu maji kupenyeza udongoni. Unaweza kulima kwa kina kirefu iwapo utaboresha jembe lako kwa kuondoa vifaa vizee na kuvibadilisha na vipya, au kutumia jembe la patasi iwapo unatumia trekta.
Matumizi ya mbolea
Weka kiwango kidogo cha mbolea samadi au mbolea ya madini kulingana na kiganja cha mkono kwa kila hatua, ukifuata mstari utakaopanda. Panda mbegu kwa umbali wa 5 cm na samadi. Usitawanye mbolea kwani hii husababisha hasara.
Iwapo unaishi eneo ambapo mvua ni kidogo, subiri hadi miche itakapopata majani 2, kisha uweke mbolea karibu na mimea iliyostawi ili kupunguza hatari ya kupoteza pesa kwa ajili ya mbolea. Iwapo mvua haitanyesha, unaweza kuamua kutonunua mbolea kabisa. Mbinu hizi zinaweza kutumiwa kwa mahindi, mikunde na mazao mengine.
Ili kufanikiwa, unahitaji mbegu bora, utunzaji mzuri wa maji, usimamizi mzuri wa rutuba ya udongo.