Malisho ya mifugo ambayo hutengenezwa kwa njia ya hydroponic ni nyongeza bora kwa chakula cha mifugo, na hivyo huongeza uzalishaji.
Malisho ya hydroponic ni chakula chenye lishe na hupunguza gharama za kulisha mifugo. Inashauriwa kuanza kwa kuhimiza mbegu kuota. Mahitaji ya kukuza malsiho haya ni pamoja na trei, maji safi, mbegu kama vile; shayiri, ngano, shayiri, mahindi na mtama.
Utaratibu
Kwanza tandaza mbegu vizuri kwenye trei safi, kisha mwagilia maji kila masaa 3–4 kwa siku.
Weka trei zilizo na mbegu kwenye sehemu ya kuoteshea, na kisha mwagilia maji kwa kwa siku 6–7.
Hakikisha kwamba trei zinazotumika zina mashimo ambayo huondoa maji ya ziada ili kuzuia mbegu kuoza.
Malisho yanapaswa kuvunwa siku ya 3 au 4 kwa ajili ya kulisha vifaranga, siku ya 6 kwa kuku waliokomaa na siku ya 7 kwa kondoo, mbuzi na ng‘ombe.