Miti ina umuhimu mwingi katika maumbile, na kupanda miti ni mbinu muhimu.
Miti hufyonza kaboni dioksidi (gesi makaa) kutoka angahewa, hutolea wanyama wa porini makazi, na pia hutoa kivuli. Unapopanga kupanda miti, amua kama lengo lako ni kupanda miti michache karibu na nyumba yako, au kujaza pengo msituni, na pia angalia nafasi uliyonayo ya kupanda miti hiyo. Mambo haya hukusaidia kufanya uchaguzi sahihi wa miti ya kupanda.
Uanzishaji wa miti
Unapoanzisha miti, eneo ni jambo muhimu la kuzingatia. Usipande miti ikikurubiana sana, wala usipande karibu na nyumba.
Unapopanda, tumia vifaa sahihi ili kurahisisha mchakato. Ikiwa una miti michache ya kupanda au una miti kwenye viriba, tumia sepetu kutengeneza shimo la kupandia. Ikiwa una miti mingi ya kupanda, sepetu maalum la kupanda miti litahitajika kwa sababu hilo lina ncha kali.
Ili kupanda, weka sepetu ardhini huku ukilishikilia, kanyaga juu yalo kwenye huku ukuliingiza ardhini hadi litakapoingia lote ndani ya ardhi. Ondoa sepetu ardhini ili kuunda nafasi ambapo mti unaweza kupandwa.
Matunzo
Baada ya kupanda, bonyeza udongo ulio karibu na mti ili uweze kuwa imara. Hakikisha kwamba mizizi ya miche ina unyevu wa kutosha hadi wakati wa kupanda.
Katika miaka michache ya kwanza, palilia ili kuondoa nyasi na magugu, na pia weka mirija ili kuilinda miche dhidhi ya wanyamapori. Unyevu ni muhimu kwa ukuaji, kwa hivyo mwagilia miche iliyopandwa