Kupogoa ni mchakato wa kuchagua na kukata sehemu na matawi ya mti. Kupogoa ni muhimu kwa sababu kunasaidia kudhibiti ukubwa wa mti, na kuweka mti kwa usawa.
Kupogoa kunapaswa kufanywa mara baada ya mavuno. Wakati wa kuvuna, vuna matunda pamoja ka mabua yake ili kuzuia mtiririko wa utomvi kutoka kwa matunda, ambayo yanaweza kusababisha uharibifu.
Kupogoa
Wakati wa kupogoa, kwanza ondoa miiba mikuu ya maua kwa sababu ni vyanzo vya mbegu za ugonjwa ambazo huoshwa na mvua na hivyo kueneza ugonjwa chini kwa mti mzima.
Tunza ukubwa wa mti kwa kuondoa matawi makubwa yasiyozaa, na pia kata ncha za matawi mengine ili yawe mafupi.
Baada ya kupogoa, mti huo hutoa majani mara moja hadi mbili, na kisha huzaa matunda tena. Baada ya kuvuna matunda, rudia kufanya tena utaratibu wa kupogoa.