Kwa kuwa ni mojawapo ya mambo yanayoathiri ufugaji wa wanyama, afya ya mnyama huamua ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana.
Ufanisi wa chanjo hutegemea uwezo wa mnyama wa kuitikia chanjo, utunzaji sahihi na jinsi ya kutoa chanjo. Chanjo huhifadhiwa kwenye chupa kulingana na kipimo kinachohitajika.
Kudunga mnyama chanjo
Chanjo hutumika moja kwa moja bila kuichanganya, na katika hali hii unapaswa kuilinda dhidi ya joto, mwanga wa jua pamoja na baridi kali inapohifadhiwa. Hifadhi chanjo kwenye jokofu iliyo kati ya nyuzi joto 35 hadi 40. Pia hifadhi bomba la sindano kwenye jokofu ambayo huzuia mwanga wa jua kuingia, pamoja na kulinda chanjo dhidi ya joto kali.
Vile vile, epuka kuchanja wakati ng‘ombe hajakauka au mchafu. Kabla ya kutumia chanjo, tikisa kwa upole au viringisha chupa ili kuichanganya ipaswavyo. Shikilia bomba ya sindano na chupa kwa mkono mmoja na tumia mkono mwingine kuondoa kipimo cha chanjo unachohitaji. Kisha chomoa sindano kwenye chupa huku ukielekeza juu, na uondoe hewa kwenye bomba la sindano.
Kabla ya kutoa chanjo kwa mnyama, mfunge na kisha uelekeze sindano mahali sahihi. Hakikisha eneo hilo ni safi.
Kwa sindano ya chini ya ngozi, tumia sindano mpya. Baada ya kubaini sehemu sahihi, vuta ngozi ya shingo ya mnyama ili kuunda mahali pa kudunga sindano huku ukiepuka kuathiri msuli. Kisha ingiza chanjo, na uondoe sindano huku ukiachilia ngozi.
Baada ya kuchanja, safisha sindano na maji ya moto, walakini usitumie dawa za kuua viini. Weka lebo kwenye kila bomba la sindano ili kuonyesha kilichomo.
Hatimaye kwa matokeo bora, chanjo inapaswa kutumika mara tu inapofunguliwa, na sindano zinapaswa kutupwa ipaswavyo kwa kufuata kanuni.