Kwa wafugaji wengi wa kuku, kutotolesha vifaranga ni changamoto kubwa.
Katika kutotolesha vifaranga, kutoa joto ni jambo muhimu kwa ukuaji wa ndege. Joto linaweza kutolewa kwa kutumia jiko la mkaa ambalo linapaswa kuwa na bomba la kuondoa moshi nje, na kama halipo jiko la mkaa liwashwe kutoka nje ya banda la kuku kwa sababu moshi huathiri mfumo wa upumuaji wa ndege.
Kushughulikia vifaranga
Wakati wa kushughulikia vifaranga, toa eneo la kutosha kulishia na kunyweshea ili kupunguza msongamano. Inapendekezwa kutolea vifaranga 50 kihori 1 cha kunyweshea na 1 cha kulishia.
Angalia halijoto la banda kwa kutumia kipimajoto au kwa kuangalia tu tabia za vifaranga. Wakati vifaranga wanahisi baridi, wanakumbatiana kwenye pembe moja karibu najiko la mkaa. Vifaranga wanapohisi joto huhemahema, hupoteza maji, na hivyo hawaongezeki uzito. Ikiwa kipimajoto kinatumika kuangalia halijoto, kinapaswa kuning‘inzwa kwenye kiwango cha urefu wa vifaranga.
Wakati wa ufuatiliaji wa halijoto, usiruhusu mabadiliko ya halijoto zaidi ya nyuzi 2 kwani hii hufanya ndege kushindwa kutoa kinyesi kwa urahisi, na ni dalili ya upungufu wa maji mwilini.
Watolee vifaranga mwanga wa kutosha, na uingizaji mzuri wa hewa.