Ni muhimu kwa wakulima kujua jinsi ya kushughulikia mbolea tofauti,ili kupata mavuno mazuri na mpunga wenye afya.
Mavuno duni yana afya kidogo na kikaboni kidogo. Maji na virutubisho hukauka na hushindwa kupokewa na mizizi. Hivyo, mimea ya mpunga hukua vibaya, hata kwa kuongeza mbolea ya madini.
Mahitaji ya Mimea ya mpunga
Unaweza kulinganisha mimea ya mpunga inayokua na kujenga ghala la matope. Kwanza una msingi, inyoamaanisha kuwa mpunga hujenga majani na matawi. Ifuatayo, ukuta na paa hujengwa, kwa hivyo mmea hutoa wimbi na maua.
Virutubisho muhimu zaidi ni nitrojeni, fosforasi na potasiamu. Fosforasi husaidia mimea kukua. Potasiamu huifanya kuwa na nguvu na husaidia kujaza mbegu. Nitrojeni hufanya mashina yenye afya na kijani kibichi, na husaidia udongo kuhifadhi maji na virutubisho. Mbolea ya madini ina kirutubisho kimoja au vyote vitatu. Una weza kujua vichanganyiko viliyomu katika mbolea fulani kwa kutizama kwa mfuko wake. »N« inasimamia nitrojeni, »P« fosforasi na »K« potasiamu. Nambari ikiwa zaidi kwa begi, humaanisha virutubisho vingi vinajumuishwa kwenye mbolea hiyo. Mbolea ya rangi ni mchanganyiko wa virutubisho. Mbolea ya Urea ina tu nitrojeni na ni nyeupe.
Kuweka mbolea katika mpunga
Mpunga unawopandwa katika nyanda za chini mara nyingi huhitaji nitrojeni, lakini una fosforasi ya kutosha na potasiamu. Mpunga unawopandwa katika nyanda za juu mara nyingi huhitaji nitrojeni na fosforasi. Maji hayawezi kuyeyusha fosforasi na potasiamu, kwaani unaweza kuiongeza wakati unapolima au kudimbua shamba. Urea huyeyuka ndani ya maji. Kwa hivyo, hufai kuiongeza kwenye shamba zilizofurika au wakati wa mvua.
Udongo wa changarawi hupoteza maji na virutubisho lakini udongo wa kitope/ mfinyanzi unavihifadhi. Mbolea kama vile samadi na mbolea oza, husaidia udongo kuhifadhi maji, virutubisho na mbolea ya madini. Palilia shamba kabla ya kuongeza mbolea ya madini, ili usilishe magugu. Ongeza urea wiki mbili baada ya kupanda au wiki moja baada ya kuatika. Ongeza urea kwa wiki mbili, kabla ya mashina kuanza kupanuka na kutoa wimbi. Tumia urea mara ya tatu wakati mpunga unapoanza kutoa maua. Jamii ya kunde kama vile mbaazi aina ya kutambaa, au soya zina nundu kwenye mizizi, ambavyo hutoa nitrojeni kutoka hewani na husaidia kurutubisha udongo.