»Kutayarisha Silage (sileji)kutoka kwa mahindi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/silage-maize

Muda: 

00:15:48
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Nawaya, UNIDO Egypt

Video hii inaeleza jinsi ya kufanya sileji kutoka kwa mahindi.

Upatikanaji wa lishe la majani mbichi

Lishe la majani mbichi hupatikana kwa wingi na thamani mbalimbali. Lishe huhitajiwa ili kulisha ng‘ombe waweze kuwa wazima na pia, watupe maziwa mengi. Wakulima wengi huwalisha ng‘ombe kwa nafaka mbalimbali na virutubisho kama chakula cha nyongeza japokua gharama yao ni kali kabisa. Uwezekano wa kuhifadhi virutubisho katika lishe kwa mwaka mzima ni kuigeuza kuwa sileji.

Uchachu

Bila ya kuingiza hewa, lishe la mahindi huweza kuhifadhiwa kwa mda mrefu bila kuoza. Vijidudu huchimba sukari inao patikana kwenye lishe , na husababisha uzalishaji wa lactic asidi amabayo husaidia kuhifadhi lishe hilo. Pia, uchachu hufanya manyasi kuwa rahisi kumeng‘enywa na ng‘ombe.

Njia bora ya kufanya sileji.

Vuna shamba lote la mahindi yakiwa yamekomaa, wakati mimea huwa yanadhihirisha rangi ya kijani. Na hapo ni hali punje za mahindi huwa na sukari ya kutosha na kusababisha mchakato wa kuchacha. Lazima, katakata mahindi yalipo karibu na makao ya ng‘ombe.

Kata majani ya mahindi ukitumia mkono au mashini kwa vipande sawa kulingana na sentimita 1-2. Vipande kadha vidogo hupendwa, yani humeng‘enyewa na ng‘ombe kwa urahisi.

Kusanya mahindi yote uliokatakata uyaweke mahali unapo tayarisha kufanyia sileji. Mahindi hayo yalipokatwakatwa, bora usiaache hewani kwa mda mrefu kwasababu huharibika.

Tandaza safu ya kwanza ya mahindi yaliokatwa kwa blanketi au mfuko. Ili kuzuwia uingizaji wa hewa, bonyeza sileji vizuri kwa kila safu unayoeka.

Endapo ukimaliza, funika sileji na plastiki . Kisha ongeza mchanga wa ukubwa wa sentimita 20 juu ya plastiki. Funika mwisho wa plastic ili kuzuwia hewa kuingia ndani ya sileji.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:51Mfugo (ng‘ombe) mmoja hula takribani kilo 25 za lishe mbichi mara mbili kila siku.
00:5201:39Lishe huhitajiwa kwa kulisha ng‘ombe ili waweze kuwa wazima na pia, watupe maziwa mengi.
01:4002:20Kama unatayarisha sileji, lishe la majani kuhifadhiwa kwa mda mrefu wa mwaka bila kuoza.
02:2103:57Lishe lilio katwakatwa huweza kuhifadhiwa bila kuoza ikiwa hewa haija penyeza ndani.
03:5804:41Lishe la majani huboresha maisha na afya ya wanyama/ mifugo.
04:4205:29Vuna mahindi yote yakiwa yamekomaa, wakati mimea haya yanadhihirisha rangi ya kijani.
05:3006:27Katakata mahindi kwa mda wa saa kadha baada ya kuvuna.
06:2807:48Kusanya mahindi yote uliokatakata uyaeke mahali unapo tayarisha kufanyia sileji.
07:4908:12Tandaza safu ya kwanza ya mahindi yaliokatwa kwa mfuko. Ili kuzuwia uingizaji wa hewa, bonyeza sileji vizuri kwa kila safu unayoeka.
08:1308:35Kwa kila safi unao ongeza, basi bonyeza sileji kwa kutumia uzito wako wa miguu.
08:3609:42Endapo ukimaliza, funika sileji na plastiki . Kisha ongeza mchanga wa ukubwa wa sentimita 20 juu ya plastiki. Funika mwisho wa plastic ili kuzuwia hewa kuingia ndani ya sileji.
09:4310:00Urefu wa rundo utapunguka kwa wiki mbili zijazo
10:0111:08Baada ya siku 45, unaweza kufunua kando ili kukagua lishe, lazima lishe lidhihirishe rangi ya hudhurungi, unyevu, na harufu tofauti.
11:0912:17Toa sileji iliooza na nyeusi
12:1813:11Hakikisha ndama hawali sileji hio.
13:1215:34muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *