»Kutengeneza jukwaa la kondoo na mbuzi lililoinuliwa«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/making-raised-platform-sheep-and-goats

Muda: 

00:08:52
Imetengenezwa ndani: 
2017

Imetayarishwa na: 

Practical Action, Bangladesh and Nepal, Christian Commission for Development in Bangladesh (CCDB).

Watu wengi ulimwenguni hufuga kondoo kwa kutoa nyama, sufu na maziwa. Katika mabanda ya kijadi, kondoo na mbuzi mara nyingi hufugwa wakiwa chini ambalo huwaweka wanyama hao katika mgusano wa moja kwa moja na mkojo pamoja na kinyesi chao. Hii husababisha usafi duni ambao hufanya wanyama wengi kupata magonjwa.

Ili kutatua changamoto hii, unaweza kuandaa jukwaa lililoinuliwa ndani ya banda lililopo ambalo linaweza kusafishwa chini yalo kwa urahisi. Jukwaa lililoinuliwa hupunguza uwepo wa magonjwa, na ni rahisi kusafisha banda, na unaweza pia kutengeneza mbolea kutoka kwa samadi.

kujenga jukwaa

Vipimo vya jukwaa huchukuliwa, miguu ya jukwaa hujengwa. Kutegemea urefu wa banda, mianzi hukatwa kwa urefu unaohitajika kufanya vigingi vya kushikilia au kuimarisha jukwaa ili kuwezesha ukusanyaji rahisi wa samadi. Ikiwezekana, jukwaa linapaswa kuwa angalau 1m juu ya ardhi.

Kata kipengo kwenye pande ya mwisho wa kigingi. Chimba shimo la kina cha nusu mita likiwa karibu na pembe ambapo unataka kuweka vigingi. Kulingana na ukubwa wa jukwaa, utahitaji kuweka vigingi vingine katikati, kila kigingi kinapaswa kuwa mita 1m mbali na kingine, na lazima vyote viwe thabiti na ngangari.

Vijiti vya mianzi huwekwa kimlalo juu ya vigingi na kufungwa kwenye kipengo kilicho katika vigingi. Mianzi iliyonyooka huchaguliwa ili kutengeneza mbao za sakafu. Mianzi hukatwa kulingana na upana wa banda.

Kupunguza uwepo wa hatari

Vifundo vikali hutolewa na husawazishwa ili wanyama wasiumizwe. Kila kijiti cha mianzi hupasuliwa katika vipande vinne sawa. kingo zilizo na ncha kali hutolewa na kusawazishwa ili kulainisha vipande vilivyopasuliwa ambavyo huwekwa juu ya vijiti vya mianzi vilivyowekwa awali kimlalo. Vipande hivyo hutundikwa kwa kila upande wa jukwaa ili kuandaa sakafu.

Kutoka kwenye vipande vilivyotundikwa, vingine hufungwa na kamba vikielekea katikati, kwa njia ambayo vinaweza kukunjwa kwa hivyo kuwezesha banda kusafishwa kwa urahisi. Mapengo hayapaswi kuachwa kati ikiwa unatumia mianzi mbichi. Ngazi ya mifuko ya mchanga hutengenezwa ili kusaidia kondoo na mbuzi kuingia na kutoka.

Jukwaa linapaswa kusafishwa kila siku ili wanyama wawe na afya.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:10Katika mabanda ya kijadi, kondoo na mbuzi mara nyingi hufugwa wakiwa chini. . Hii husababisha magonjwa.
01:1102:12Jukwaa lililoinuliwa linaweza kusafishwa kwa urahisi, na hivyo hupunguza uwepo wa magonjwa, Vile vile, samadi yao hutumiwa kama mbolea
02:1303:30Jukwaa hilo linajengwa kwa kutumia mianzi. Miguu yake huinuliwa angalau 1 m juu.
03:3003:52Vigingi au fito huwekwa kwenye mashimo kwenye pembe nne kwa muachano wa 1m.
03:5305:00Vijiti vya mianzi huwekwa kimlalo juu ya vigingi. Kila kijiti cha mianzi hupasuliwa katika vipande vinne sawa.
05:0105:43Vipande vya mianzi hufungwa kwa kila upande na kamba vikielekea katikati, kwa njia ambayo vinaweza kukunjwa kwa urahisi.
05:4406:18Mapengo hayapaswi kuachwa kati ikiwa unatumia mianzi mbichi
06:1807:08Ngazi ya mifuko ya mchanga hutengenezwa ili kusaidia kondoo na mbuzi kuingia na kutoka. Jukwaa linapaswa kusafishwa.
07:0807:40Kwa kutumia vifaa vya ujenzi vya kienyeji, tunaweza kujenga jukwaa lililoinuliwa kwa urahisi bila kutumia pesa nyingi.
07:4108:52Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *