Sileji ni lishe bora kwa mbuzi linalotengenezwa kwa urahisi kutoka kwa mahindi ya manjano, na nyasi nyingine zilizoboreshwa. Hata hivyo, hewa inapoingia silaji huoza. Kupitia hatua zinazofaa, sileji yenye ubora inaweza kutayarishwa kwa urahisi.
Sileji hudumu kwa siku 15 hadi miaka 2. Hata hivyo, tumia chacha ili kuongeza virutubisho kwenye sileji, na hivyo kusababisha ukuaji bora wa mbuzi. Linda sileji dhidi ya mvua, maji, na panya kwani hizi zinaweza kupunguza ubora wake. Hakikisha kuna unyevu kwenye lishe kwa takribani 60% hadi 65%.
Hatua za kufuata
Kwanza, panda mahindi ya manjano na uyavune pamoja na gunzi zake baada ya siku 85. chimba mashimo, na kisha utengeneze kuta na sakafu za saruji ndani yamo ili kudhibiti panya. Kisha weka damani za plastiki kwenye pande za shimo ili kuhifadhi unyevu, na kuzuia hewa na maji kuingia kwani hizi huharibu sileji kwa urahisi. Pia kata malisho katika vipande vidogo ili viweze kushinikizwa kwa urahisi, kuhifadhi kwa urahisi, na kurahisisha ulaji kwa wanyama. Inashauriwa kuchanganya lishe na mimea ya mikunde ili kuboresha sileji.
Baada ya hayo, yeyusha na uchanganye kilo 20 za sukari guru kwenye lita 150 za maji, na 250g ya chacha ya silaji. Kisha nyunyiza kwenye malisho ili kuongeza ubora na usagaji wa chakula. Ongeza kilo 1 ya chumvi kwa tani moja ya malisho ili kuboresha ladha. Jaza ghala kwa siku hiyo hiyo. Kisha vuna na ukate malisho pamoja na nafaka zake kwa kudumisha afya ya wanyama na kuepuka matumizi ya chakula kinachonunuliwa dukani.
Tumia mbolea ya kikaboni, na badilisha mazao ili kuongeza rutuba ya udongo. Mahindi ya manjano hayawezi kustawi vyema katika mvua nyingi, na udongo wenye rutuba kidogo.