Asali ni biashara nzuri. Asali huhitajika kwa sababu ya umuhimu wa lishe yake.
Katika mizinga ya kienyeji, kuvuna asali ni ngumu kwani nyuki hutengeneza masega yao ambayo mara nyingi huambatana. Katika mzinga wa kisasa, asali hutolewa kwa kutumia kifaa cha kuvunia. Kisha asali hukusanywa bila kuharibu masega, na hivyo kuokoa wakati na nguvu zingezotumika kujenga masega mapya.
Ili kutengeneza mzinga, tumia vipande vya mbao ambavyo havipotoshi kwa urahisi, haviozi, havina harufu yoyote mbaya, na ni vyepesi.
Kutengeneza mzinga wa nyuki
Ili kutengeneza mzinga wa nyuki, chagua vipande vya mbao vyenye unene wa sentimita 2, urefu wa 50cm, upana wa 46cm na urefu wa 26cm kwa pande zote mbili. Lainisha usoni wa ndani ili kuhakikisha kuwa nyuki hawapotezi wakati kulainisha. Weka vigingi viwili chini ya mzinga ili kuupa msimamo.
Tengeneza mlango wa kuingilia uliye na upana wa cm 11 na urefu wa cm 0.8 kwa upande wa chini wa mbao kidogo ili kuruhusu nyuki kuingia, na kuzuia nyigu na wadudu wengine. Acha sehemu iliyopanuliwa kulingana na 5cm chini ya mlango ili nyuki waweze kupafikia kabla ya kuingia kwenye mzinga.
Tengeneza fremu ambazo nyuki watatumia kama muongozo wa kuweka masega yao. kwa kila fremu, kata vipande vidogo vya mbao viwili vilivyo na urefu wa 21.6 cm, unene wa 2cm, na upana wa 4 cm. Vipande vidogo vya mbao ambavyo vinawekwa kwa pande zote mbili vinafaa kuwa na muundo kama wa manati ili nyuki waweze kupata nafasi ya kutosha kutembelea kati ya masega. Weka waya kupita kwenye mashimo yaliyo kwenye fremu, tumia msumari kuthibitisha waya kwenye fremu.
Kutunza nyuki
Nyuki huhitaji joto lakini hawawezi kufanya kazi vizuri iwapo hali ya joto ni moto sana. Weka kifuniko kinachoweza kuondolewa ili kutatua shida hii. Funika kifuniko na bati, na uache upande udogo wazi huku ukifunikwa kwa wavu ili kulinda mizinga kutokana na wanyama waharibifu, jua na mvua.
Piga rangi nyeupe nje ya mizinga kwani rangi zingine nyeusi zinaweza kuwapuuza nyuki.
Weka mizinga yako juu ya ardhini, kwenye kivuli wakati wa kiangazi, na uziweke juani wakati wa msimu wa baridi.