Tende mbichi huuzwa bei duni sokoni, na hudumu kwa muda mfupi baada ya kuvunwa. Tende huharibika baada ya muda. Kushinikiza tende huongeza thamani ya tende sokoni, pamoja na kuwezesha tende kuhifadhiwa kwa muda mrefu.
Tende huiva kwa nyakati tofauti. Kwa hivyo, wakati wa kuvuna, tikisa matawi kwa upole ili kuchuma tende zilizoiva. Mwishoni mwa msimu, kata matawi yaliyoiva kabisa na uondoe tende kwa kutumia mikono. Ili kuandaa tende zilizoshinikizwa, lazima tende zinafaa kuwa zimekomaa na kuiva kwa usawa. Kukaushia tende chini ya jua kunaziwezesha kupata ukomavu unaofaa ili kushinikizwa, na pia husaidia kupunguza unyevu wa tende. Wakati wa kukausha tende, kausha kila mavuno mapya kivyake.
Usafi wakati wa kushinikiza
Chagua siku iliyo na joto kali ili kushinikiza tende. Anza mchakato wa kushinikiza saa sita za mchana baada ya tende kupokea jua la asubuhi. Weka vyombo vya kufungasha kwenye mahali safi katika eneo la kukaushia. Chombo cha kufungasha kinafaa kuwa na ukingo mkubwa wa kutosha ili kurahisisha mchakato wa kushinikiza tende, na kinafaa kuwa rahisi kubebwa mara baada ya kujazwa.
Weka mfuko wa plastiki usiopenyeza hewa kwenye kreti iliyotengenezwa kwa majani ya mitende. Karatasi huwekwa ndani ya kreti ambayo hupanuliwa na kiunzi cha mbao kinachoweza kuondolewa. Karatasi huzuia uharibifu kwa mfuko wa plastiki, na kiunzi huimarisha kreti wakati wa kushinikiza tende.
Suuza tende kwenye kikapu ukitumia maji safi na uondoe tende zilizoharibika, matawi au mawe. Tikisa kikapu ili kuondoa maji yoyote ya ziada. Mimina tende kwenye mfuko wa plastiki kwa mafungu madogo wakati ukishinikiza. Ongeza safu nyingine ya tende wakati ile safu ya awali imeshinikizwa vizuri na kusawazishwa. Funga vizuri mfuko wa plastiki ikiwa umejaa.
Ondoa kiunzi cha mbao na ongeza safu ya karatasi ya mwisho, na ufunge vizuri kifuniko kwenye kreti ukitumia waya. Kisha, hifadhi tende chumbani bila kugusa ardhi. Panganya kreti za tende hadi tabaka 3, lakini ikiwa utazihifadhi zaidi ya miezi 2, badilisha kreti ya chini na ile iliyo juu.