Nzi wa matunda ni moja wapo ya wadudu ambao huharibu sana matunda ulimwenguni kwote. Hata hivyo, teknolojia zaidi zimebuniwa kupunguza tatizo hilo.
Nzi hao husababisha uharibifu kubwa katika matunda kwa kutaga mayai yao ndani ya ngozi ya matuda. Mayai hayo yanapoanguliwa, mabuu (minyoo myeupe) ambayo hotokea husababisha uozo. vyambo vinavyotumiwa kudhibiti nzi wa matunda ni pamoja na: chakula kilicho na protini nyingi, na sukari ambavyo huhitajika kwa nzi ili waweze kustawi, kukua na kutaga mayai. Nzi wa matunda wanaweza kunusa chakula kutoka umbali wa mita 10. Baadhi ya vyambo vya kununuliwa huwa na harufu inayoweza kuwavutia nzi kutoka umbali mkubwa zaidi. Tumia chambo cha kununuliwa kilichochanganywa na dawa ya kuua wadudu.
Mitego ya pheromone (harufu za hisia za wadudu)
Chambo hutumiwa kama dawa ya kunyunyiza. Walakini, tumia mitego ya pheromone kukagua uwepo wa nzi. Nzi huonekana maembe yakiwa na upana wa 3m. Mara baada ya kugunduliwa, changanya maji na chambo kwa uwiano wa lita 3:1. Rekebisha tundu la mrija wa kunyunyizia na unyunyize dawa katika upande wa juu na chini ya majani kwa kila mti, na kwa upana wa mita 1 kwa 1. Dawa hufanya kazi kwa angalau siku 10 baada ya kunyunyizwa. Usinyunyize dawa siku iliyo na upepo. Nyunyiza tena bada ya mvua kubwa. Nyunyiza asubuhi wakati nzi huwa na shughuli sana.
Kulinda chambo dhidi ya mvua
Kata chombo cha manjano kati kati kisha upake chambo kinachonata ndani yake. Ninginiza chombo kwenye mti upande uliyokatwa ukiangalia chini ili kuzuia chambo kunyeshewa na mvua. Loweka sponji kwenye chambo cha chakula, na uifungie chini ya kifuniko ili isinyeshewe. Ninginiza sponji hii kwenye mti. Tumia mbinu nyingine za kudhibiti nzi pamoja na chambo cha chakula. Mbinu hizi ni pamoja na ; kuokota na kuharibu matunda yaliyoanguka, na kuhimiza uwepo wa madui asili wa nzi kama vile koyokoyo. Chambo hakiui wachavushaji wa mbegu za maua.