Koyokoyo (siafu wekundu) husaidia sana kupunguza hasara zinazosababishwa na nzi wa matunda kupitia njia kadhaa.
Nzi wa matunda ni wadudu waharibifu sana ambao hutumia ncha zao zilizoelekezwa kutaga mayai ndani ya ngozi ya matunda. Mayai hayo huanguliwa kuwa minyoo (mabuu) ambayo husababisha matunda kuanguka. Walakini ni muhimu kubainisha kati ya madoa yanayosababishwa na asidi isiyo hatari ambayo hutolewa na koyokoyo, na madoa hatari meusi yanayosababishwa na nzi. Vile vile, hakikisha unachuma matunda mapema ili kupunguza uharibifu.
Jinsi koyokoyo hulinda matunda
Koyokoyo hufukuza, kushika, na pia kuwala nzi wa matunda. Koyokoyo pia hushuka chini na hutamba ardhini ili kutafuta chakula kwa matunda yaliyoanguka. Wao huwasiliana kwa kutoa harufu ambayo hutisha na kufukuza nzi wa matunda.
Vinginevyo, tumia mbinu za kuhimiza koyokoyo pamoja na mbinu nyingine kama vile mitego ya nzi wa matunda, kuokota na kuharibu matunda yaliyoanguka ili kuondoa nzi katika matunda na kuongeza mavuno.
Unafaa kujipaka jivu ili mwili wako uteleze kwa koyokoyo yaani wasikupande kusababisha madhara.