Unaweza kuua viwavijeshi kwa kutumia njia ya asili ili kulinda mahindi dhidi ya wadudu hawa.
Viwavijeshi hula majani ya mahindi. Mara nyingi vidudu hawa hutoboa mashimo makubwa kwenye majani, na hula mpaka gunzi la mahindi. Viwavijesha waweza kuwa wadudu wa kutambaa wakiwa wachanga , au mayai ambayo kwamba wanageuka nondo wakikua.
Usaidizi wa kiasili
Asili huwapa wakulima njia kadha nyingi za kuzuia viwavijeshi dhidi ya shamba za mahindi. Wasaidizi hawa huitwa vidudu marafiki wa wakulima, nakadhali wanaweza kuwaua zaidi ya nusu ya viwavijeshi walio shambani. Kobe au bunzi na nyigu hula mayai ya viwavijeshi. Na pia ndege, popo na buibui hula nondo.
Wakulima wanapo nyunyiza dawa ya kuua viwavijeshi, idadi nyingi ya wadudu marafiki wa wakulima hufa. Zaidi ya hayo, dawa hizo hazifiki ndani kabisa kuwaua viwavijeshi wanao jificha. Kwa hivyo, ni muhimu kutumia mbinu bora za kiasili kuliko dawa.
Kupunguza viwavijeshi
Tumia mikono kuua viwavijeshi na mayai hadi mimea yatakapofika mwezi 6 ya kwanza, kwa sababu huu ndio wakati hatari zaidi kwa mimea.
Ili kuvutia chungu ambao kwamba huwadhibiti viwavijeshi, pakaa mafuta ya kupikia kwenye shina la mahindi yakiwa yamefika urefu wa magoti. Pakaa mafuta katika sehemu ya chini ya shina na mita moja kuenda juu wakati mahindi yanapo zaliwa. Panda miti, maua na vichaka karibu na shamba lako ili uwape wadudu marafiki wa wakulima sehemu ya kuishi.
Pia, unaweza kupunguza idadi ya viwavijeshi shambani kwa kutumia mchanganyiko wa asili maalum. Unacho hitaji ni: majani ya mbangi mwitu, majani ya mtupa, pilipili iliyoiva na majani ya mshubiri yote kulingana na kipimo cha mkona .
Katakata mimea yote kisha uiweke kwenye mtungi ulivyo na lita 6 ya maji uichemushe kwa takribani saa moja nzima. Kisha aacha mchanganyiko huo upowe kabla ya kuichuja. Ongeza ugoro kisha ukoroge kwa kama dakika 5. Chuja mchanganyiko huo tena kwa mara kadha. Baada ya kujaza mchanganyiko kwenye mtungi wa lita 5, funga kisha uiweke chini ya kivuli. Siku ifuatayo, toboa shimo ndogo kwenye kifuniko cha mtungi ili gasi iweze kutoka. Iache ichace kwa wiki mzima. Hapo, unaweza kutumia mchanganyiko huo. Ongeza maji lita 20 kwenye lita 1 ya mchanganyiko ambao kwamba unaweza kunyunyizia nusu ya hekteya ya shamba la mahindi.