Siagi ya Shea bora ni chanzo kizuri cha mapato. Walakini, uvunaji na utunzaji duni wa karanga shea husababisha mbegu duni ambazo husindikwa kuwa siagi ya shea.
Matunda ya Shea huchachushwa ili kuondoa karanga kwa urahisi.
Kukausha na kuhifadhi
Kusanya karanga za shea zilizokomaa kabisa ambazo zimeanguka ardhini kwenye vyombo safi ili kupata nafaka bora. Ondoa karanga kutoka kwa tunda la Shea mara tu ili zisichache.
Kwa kuongeza, kausha karanga kwa siku 3–5 kwenye maturubai safi au mkeka: Angalia kiwango cha ukaushaji kwa kutikisa mbegu mkononi. Ikiwa zimekaushwa vizuri, hutoa sauti maalum. Mara tu, pukuchua karanga kwa kuzipiga lakini usiziponde, kisha chagua punje na kuzichambua kulingana na ubora. Baada ya kuchambua , fungasha punje kwa mifuko tofauti ukiweka kiasi nusu ili kuzuia joto lingi kutokea ambalo linaweza kusababisha ukungu. Mwishowe, hifadhi mifuko hiyo kwa hali ambapo hazigusi ardhi ili punje zisipate unyevu na zikaharibika.