Ili kupata mavuno bora, ni muhimu kujua njia mbalimbali za kudhibiti mahindi kwa sumukuvu baada ya kuvuna.
Mahindu yanaweza kupata kuvu na ukungu yakiwa hayakukaushwa na kuhifadhiwa vizuri. Kuvu hizi hutoa sumu inaitwa sumukuvu. sumukuvu huathiri maisha yetu. Kwani wanyama na watu hawafai kula mahindi yalio athiriwa na sumukuvu, kwa sababu wanyama wakila lishe au chakula kina sumukuvu, sumu hii hupatikana hadi katika maziwa, mayai na nyama. Kwahivyo, mtu pia huathiriwa akikula bidhaa hizo.
Nafaka eneye kuvu/ ukungu.
Ukihifadhi mahindi kabla hayajakauka kabisa, nafaka huvunjika na unyevu huingia. Unyevu ukiingia, sumukuvu huvamia nafaka hizo. Yaani ni muhimu kabisa kukausaha mavuno kabla ya kuyahifadhi. Lakini hata kwa kuhifadhi, kuvu huvamia mahindi yakiwekwa kwa ardhi.
Kukausha na Kuchambua mahindi
Chagua mahindi ya rangi tofauti wakati wa kuvuna. Kama pande moja la mahindi limevamiwa, basi litowe.
Kama mahindi yamevunwa na kukusanyiwa, basi yalinde dhidi ya mvua. Tandaza punje za mahindi kwenye mkeka, hema au jukwaa safi, uziache zikauke kwa wiki kadha. Geuza mahindi mara kwa mara kisha uyafunike usiku. Punje zamahindi zikianza kulegeza wakati wa kugeuza, basi jua kwamba mahindi yamekauka kabisa.
Kuhakikisha kwamba punje zimekauka vizuri, ziweke kwa hema au turubai mara tena, kisha uyakaushe mahindi kwa siku kadha. Hakikisha kwamba safu ya mahindi inaoanikwa kwa hema isizidishe urefu wa nusu ya kidole.
Wakati unapo geuza punje za mahindi, hakikisha kwamba hayapati unyevu.
Ili kuhifadhi mahindi vizuri, tumia mbinu ya chumvi na chupa, na kama mahindi yamekauka vizuri, basi yahifadhi kwenye mahali safi isiopenyeza hewa. Pia, mahindi yanayohifadhiwa, lazima yasiguse paa, sakafu wala ukuta.