Muhogo una uwiano mdogo wa kuzidisha, lakini kuzaliana kwa haraka husaidia kuongeza mavuno ya jumla ya muhogo.
Uwiano wa kuzidisha uzalishaji ni ongezeko la vipandikizi kulingana na vile vilivyopandwa. Kuzidisha kwa haraka katika muhogo hufanywa kwa kukata vipandikizi vidogo vya shina. kipandikizi kidogo cha shina ni kipande kidogo cha shina ambacho kina fundo moja au zaidi kulingana na sehemu ya shina kilichokatwa. Wakati wa kukata, tumia vifaa vikali ambavyo ni pamoja na cutlas, mkasi, na msumeno.
Vipandikizi vya shina
Shina la muhogo limegawanywa katika sehemu tatu ambazo ni pamoja na; sehemu ya mbao ngumu, sehemu ya mbao isio ngumu, na sehemu ya ncha. Vipandikizi kutoka kwenye sehemu ya mbao ngumu vinapaswa kuwa na fundo moja au mbili. Vile vya sehemu zisizo ngumu vinapaswa kuwa na urefu wa futi moja. Kwa vile vya sehemu ya ncha, ondoa majani yote lakini jihadhari usiharibu vichipukizi (vijicho), na uweke vipandikizi mara moja katika maji ili kuvizuia kunyauka.
Idadi ya vipandikizi kutoka kwenye shina moja inategemea urefu wa shina, kipenyo cha shina, umri wa mmea na hali ya hewa wakati na baada ya kupanda. Vipandikizi 60 hadi 100 vidogo vinaweza kupatikana kutoka kwa shina moja.
Matibabu ya shina
Kabla ya kupanda, tibu vipandikizi vya muhogo kwa dawa ya kuua kuvu. Fanya hivyo kwa kutumbukiza vipandikizi kwenye dawa ya kuua kuvu na viache vikauke kidogo kabla ya kupanda.