Mnyororo wa thamani wa kilimo unajumuisha kila mtu anayefanya kazi ili kupata mazao kutoka kwa mkulima hadi kwa mlaji. Kila mtu aliye katika mnyororo huu ni muhimu.
Mkulima anapotumia mbinu duni za uzalishaji kama vile; kupanda mbegu zisizo bora, kunyunyizia dawa hatari za wadudu, kutopepeta vizuri mahindi wala kuyakausha, na pia kutoyahifadhi vizuri pamoja na kuongeza mawe na taka kwenye mifuko ili iwe nzito, hupata bei ndogo kutoka kwa mfanyabiashara anapouza mazao yake kutokana na ubora duni wa mazao.
Wafanyabiashara na msagaji
Mfanyabiashara anapouza mahindi kwa msagaji, msagaji pia humpa mfanyabiashara bei ya chini na mfanyabiashara hapati faida yoyote. Msagaji husafisha, hukausha na kusindika mahindi kuwa unga. Mnunuzi hununua unga na kwenda nao nyumbani lakini familia haipendi ladha ya unga huo na kumwacha mtoto mmoja akiwa mgonjwa. Hii hudhuru wanachama wote walio katika mnyororo wa thamani.
Kuongeza thamani
Lakini mkulima anaponunua mbegu bora na kutumia dawa nzuri anapata mavuno mengi na anapokausha mahindi, akayapepeta na kuyahifadhi vizuri na kuamua kuuza na wakulima wengine baada ya kufanya utafiti wa soko kujua taarifa za soko, hupata bei nzuri kutoka kwa mfanyabiashara. Kisha mfanyabiashara huuza mahindi kwa msagaji kwa bei nzuri ambaye husaga mahindi na kuyauzia wanawake wengi kwa bei nzuri, wanawake hupikia familia zao chakula na kila mmoja hupenda chakula hicho. Hapa kila mmoja katika mnyororo wa thamani hufurahia.
Hili linawezekana mbinu nzuri zinapotumika katika uzalishaji, usafirishaji, uhifadhi na usindikaji wa bidhaa, pamoja na wakati wakulima, wafanyabiashara na wasagishaji wanashirikiana kujenga uaminifu na wakati wanapokuwa na taarifa za soko.