»Maandalizi ya shamba la mpunga«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/node/3358

Muda: 

00:10:22
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

AfricaRice, Agro-Insight, Countrywise Communication, INERA

Kuandaa na kusawazisha shamaba mara mbili kutasaidia mpunga wako kuota vizuri na kuwa na afya. Hii huboresha mavuno yako.

Kwenye shamba ambalo halijasawazishwa vyema, magugu zaidi huonekana katika sehemu za juu na lazima usubiri kwa muda mrefu kwenye sehemu za chini kabla ya kuanza kuatika. Miche mikubwa hutoa matawi vibaya, na kutoa mavuno kidogo. Kwenye shamba lisilosawazishwa, mbolea ya madini inakaa kwenye sehemu za kina na mpunga pia hautakuwa sawa. Mpunga uliyo kwenye sehemu za juu hukomaa mapema kuliko ule uliyo kwenye sehemu za chini zaidi.

Kuandaa mashamba ya mpunga

Utayarishaji mzuri wa shamba utalegeza mchanga na kurahisisha kumwagilia maji na mipito ya maji. Pia huruhusu kunyonya mbolea kwa urahisi. Kwa kuongezea, maji ya umwagiliaji huenea sawasawa, shamba likisawazishwa vizuri.

Safisha shamba lako na ukate magugu madogo na mabaki ya mazao. Kisha ueneze haya toye kwenye shamba. Ili kuufanya mchanga kuwa laini zaidi, na pia lowesha maji shambani mara mbili kwa siku mbili hadi tatu.

Fanya kilimo cha kwanza wiki chache kabla ya kupanda au kuatika, kwa hivyo magugu na mabaki ya mazao yanaweza kuoza. Waweza kutumia jembe,mashine au kifaa kinacho vutwa na wanyama. Hii hugeuza na kufungua udongo ili uwe mwepesi. Changanya majani ya mpunga na mabaki mimea mingine ili kuharakisha kuoza. Vunja udongo uliyoshikamana na pia ongeza uhusiano wa maji na udongo.

Lowesha maji shambani kwa kiwango cha sentimita mbili (2), kwa muda wa wiki mbili hadi tatu. Utapata manufaa ifuatayo; wadudu watawawa, na mabaki ya mimea itaoza. Pia hufanya magugu kuoza. Baada ya kumwagilia shamba, unafaa kuongeza mbolea ya madini na mbolea ya nyumbani. Mbolea za numbani zinaweza kuwa takataka, samadi ya mifugo na mbolea oza. Ikiwa unatumia mbadala zaidi ya mbolea ya nyumbani, unahitaji mbolea kidogo ya madini.

Waweza kutayarisha shamba lako kwa mara ya pili kwa kugeuza udongo, kuua magugu na kusambaza virutubisho. Kwa hivyo lima kina cha sentimita 10 hadi 15. Ukilima kidogo, haitaweza kusaidia mimea yako kukua. Lakini ukilima zaidi, mbolea inaweza kuwa mbali kuliko mizizi ya mimea.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:41Utangulizi
00:4200:59Kuandaa na kusawazisha kutasaidia shamba lako.
01:0001:56Utayarishaji mzuri wa shamba utalegeza mchanga na kurahisisha kumwagilia maji na mipito ya maji
01:5702:50Kwenye shamba ambalo halijasawazishwa vyema, magugu zaidi huonekana katika sehemu za juu na lazima usubiri kwa muda mrefu kwenye sehemu za chini kabla ya kuanza kuatika.
02:5103:21Kwenye shamba lisilosawazishwa, mbolea ya madini inakaa kwenye sehemu za kina na mpunga pia hautakuwa sawa.
03:2204:52Safisha shamba lako na ukate magugu madogo na mabaki ya mazao
04:5305:14Waweza kutumia jembe,mashine au kifaa kinacho vutwa na wanyama.
05:1505:24Vunja udongo uliyoshikamana na pia ongeza uhusiano wa maji na udongo.
05:2505:31Fanya kilimo cha kwanza wiki chache kabla ya kupanda au kuatika, kwa hivyo magugu na mabaki ya mazao yanaweza kuoza
05:3205:49Lowesha maji shambani kwa kiwango cha sentimita mbili (2), kwa muda wa wiki mbili hadi tatu.
05:5005:53Acha magugu kuchipua au kuoza
05:5406:51Baada ya kumwagilia shamba, unafaa kuongeza mbolea ya madini na mbolea ya nyumbani.
06:5207:23Waweza kutayarisha shamba lako kwa mara ya pili kwa kugeuza udongo, kuua magugu na kusambaza virutubisho
07:2408:55sawazisha shamba
08:5609:53Muhtasari
09:5410:22Credits

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *