Soya imethithiri protini. Mbinu bora za kilimo husababisha mazao mazuri.
Soya hulimwa kwenye aina mbalimbali za udongo, na hunawiri sana kwenye udongo ulio na muundo mzuri, na mboji ya kutosha.
Mboji huunda udongo wenye rutuba ulio na kina kirefu, ambao huhifadhi maji.
Udongo wa changarawe na mchanga hukauka kwa urahisi. Soya hutatizika kuota kwenye udongo uliyoganda.
Maandalizi ya ardhi
Kutayarisha ardhi vizuri huhimiza uotaji mzuri, hupunguza uvamizi wa magugu, wadudu na magonjwa.
Pima rutuba ya udongo ili kubaini virutubisho vinavyokosekana ili viweze kuongezwa.
Lima ardhi ili kuondoa magugu, lainisha udongo ili kurahisisha kupanda. Kamwe usichome mabaki ya mimea shambani kwani huku kunafanya ardhi ibaki wazi na hivyo kusababisha mmomonyoko, kupunguza uzazi na kuharibu rutuba ya udongo.
Vunja na kulainisha mabonge ya udongo ili kupanda.
Kata mimea yote kwa jembe, mafahali au trekta ili kuboresha mboji. Tumia dawa za kuua magugu ili kuondoa magugu yote kabla ya kulima.
Panda kwenye kitalu tambarare au kwenye matuta katika mashamba yaliyo katika nyanda za maji.
Safisha mazingira ya shamba lako. Maeneo haya yanaweza kuvutia wadudu na panya ambao huharibu mazao.