»Maharagwe kama mazao ya relay«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/beans-relay-crop

Muda: 

00:13:20
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Tv-Agro-CentroAmerica

Ukitaka kuzidisha mavuno ya maharagwe, unafaa kufanya umbali mzuri kati ya mimea, kutumia mbolea na kupanda aina zilizothibitishwa.

Maharage mara nyingi huvunwa katika nusu ya pili ya msimu wa mvua. Hii husababisha, kuwa mavuno ni machache. Pia unaweza kufanya hasara kubwa ya maharagwe yaliyohifadhiwa kwa sababu ya shambulio la wadudu au ukungu.

Kuzalisha maharagwe

Ukipanda maharagwe kama mazao ya relay baada ya mahindi, unafaa kuacha nafasi ya sentimita 25 kati ya kila safu ya mmea. Panda mbegu 2 au 3 kwenye kila tuta. Panda safu 2 za maharagwe katika kila safu ya mahindi. Dari ya maharagwe haifai kufunikwa kabisa, ili magonjwa yasisambazwe kwa mimea mingine

Maharagwe hujitengenezea mbolea ya nitrojeni na mizizi, kwa hivyo ni muhimu kwamba mizizi ikue vizuri. Kwa ukuaji uzuri, mizizi huhitaji fosforasi (Phosphorous), kwa hivyo tumia mbolea . Baada ya mbolea kuzikwa ndani ya ardhi, huenda kwenye maharagwe. Ili kufanya mchakato uwe rahisi, unaweza kuichanganya na maji.

Kuhifadhi maharagwe

Baada ya kuvuna, unafaa kukausha maharage na kuyaweka pamoja na makapi yao kwenye mifuko. Ili kuhakikisha kuwa wadudu hawapati njia ya kuingia, tumia magunia 3.

Ili kuhifadhi maharagwe kwenye ghala la chuma, safisha ghala hilo na ulijaze na maharagwe safi. Kisha ongeza vidonge. Kwa paundi 300 za maharagwe tumia kidonge kimoja. Weka vidonge kwenye vikombe vinavyoweza kutupwa ili visichanganyike na maharagwe. Kisha, funga ghala kwa kukaza na mkanda au mpira.

Wadudu hutaga mayai yao kwenye maharagwe wakati maharagwe bado yapo shambani. Mayai haya huharibiwa na vidonge vilivyoekwa kwenye ghala la chuma. Ghala halifai kuwa na mashimo au matundu, ili wadudu wapya wasiingie.

Baada ya siku 12 unatoa vidonge nje na kuvizika mara moja, kwa hivyo watoto au wanyama wasipate sumu. Wakati wowote unapofungua ghala hakikisha kwamba unaifunga haraka tena, ili wadudu wasiingie.

 

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:41Chukua aina zilizothibitishwa
01:4201:49Acha nafasi ya sentimita 25 kati ya kila safu na mmea.
01:5001:54Panda mbegu 2 au 3 kwenye kila tuta.
01:5502:25Panda safu 2 za maharagwe katika kila safu ya mahindi.
02:2603:05Dari ya maharagwe haifai kufunikwa kabisa, ili magonjwa yasisambazwe kwa mimea mingine
03:0604:00Zika mbolea
04:0105:05Ili kufanya mchakato uwe rahisi, unaweza kuichanganya na maji.
05:0605:54Fukuzi hutaga mayai shambani kwa majani ya maharagwe.
05:5506:40Kausha maharage na kuyaweka pamoja na makapi yao kwenye mifuko 3
06:4107:45Hifadhi maharagwe katika ghala la chuma
07:4610:43Weka vidonge katika chupa, juu ya ghala kisha ulifunge kwa nguvu.
10:4410:56Baada ya siku 12 toa vidonge nje na kuvizika mara moja
10:5711:19Wakati wowote unapofungua ghala hakikisha kwamba unaifunga haraka tena, ili wadudu wasiingie.
11:2013:20Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *