Kupanda mseto ni sehemu kuu ya kilimo cha miti na mazao na kuna mbinu ambazo zinapaswa kufanywa ili kupata matokeo bora kutoka kwa kilimo mseto.
Kupanda mazao ya kudumu kama kahawa, kakao au miti ya matunda huongeza manufaa ya kiuchumi na kijamii. Michanganyiko mahususi ya miti inaweza kuchukuliwa na wakulima kulingana na mahitaji yao, mazingira na upatikanaji wa soko. Upandaji mseto unaofaa unategemea sifa za eneo, mazingira na upendeleo wa mkulima.
Uchaguzi wa mazao ya kilimo mseto
Uchaguzi wa mazao ya kilimo mseto hutegemea upendeleo wa mkulima na uwezo wake wa kupata vibaru na muda. Wakati wa kutengeneza mpango wa matumizi ya ardhi, chagua miti na mazao yanayofaa, lakini pia zingatia mpangilio wa upandaji na usimamizi ili kupunguza ushindani kati ya vipengele vya kilimo.
Mikahawa inaweza kupandwa mseto na mazao kama vile, viungo au matunda kwa safu sambamba au kwenye mpaka wa shamba. Kupanda mseto na mikunde huongeza nitrojeni ambayo inaweza kutumika na mikahawa.
Kakao mara nyingi hupandwa mseto pamoja na mahindi, mihogo, papai na migomba. Mimea hii haitoi chakula tu bali pia kivuli kwa miche michanga hivyo basi kupunguza vifo vya mazao.
Mambo ya kuzingatia unapopanda mseto
Tolea mimea kivuli kwani hiki ni muhimu kwa afya ya zao. Pia punguza ushindani wa maji na virutubisho.
Tolea mimea mbolea pamoja na kudhibiti wadudu.
Ili kupanda mseto katika shamba lililopo, kwanza ondoa miti isiyozaa. Pogoa miti pamoja na kupunguza idadi ya miti ilyo shambani ili kuunda nafasi zaidi ya mseto. Chagua mazao ya mseto kwa kuzingatia upendeleo, fursa za soko, hali ya hewa na sifa za udongo. Kwa usimamizi rahisi, panda mazao mapya kwa njia iliyopangwa pamoja na umbali wa kupandia uliopendekezwa.