Usimamizi wa ngombe wa maziwa katika majira ya kiangazi inahusisha mbinu kadhaa zinazopendekezwa kufuatwa ili kupunguza athari zinazotokana na kiangazi.
Joto lingi kwenye mabanda ya mifugo husababisha mafadhaiko kwa wanyama na hivyo kupunguza kiwango chao cha uzalishaji wa maziwa, magonjwa na hasara kubwa. Kwa hivyo inashauriwa kuhakikisha usimamizi mzuri mifugo katika wa majira ya kiangazi ili kuunda mazingira mazuri kwa mifugo.
Kupunguza joto
Daima jenga mabanda ya wanyama yaliyo na uingizaji mzuri wa hewa katika uelekeo wa mashariki-magharibi ili kupunguza mafadhaiko yanayotokana na mwanga mwingi wa jua.
Tumia mfumo wa kupunguza joto kama vile vivuli, feni, viyoyozi, vinyunyuziaji ili kupunguza mafadhaiko yanayotokana na mwanga mwingi wa jua.
Wape wanyama lishe mbichi asubuhi na jioni.
Chimba vidimbwi ya maji karibi na shamba kwa ajili ya wanyama kuogelea wakati wa joto.