»Mbolea za kibaiolojia«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=QV-kIt6wHok

Muda: 

00:06:50
Imetengenezwa ndani: 
2014

Imetayarishwa na: 

Shramajeevi TV

Mbolea ya kibaiolojia ni kichocheo cha asili cha rutuba ya udongo ambayo hupatikana rahisi kwa wakulima.

Mbolea ya kibaiolojia ni mchanganyiko wa viumbe vidogo vinavyotolea mimea virutubisho. Rhizobium ni mbolea maarufu zaidi ambayo huishi kwenye vinundu vya mimea na huongeza takribani kilo 20–50 za nitrojeni kwa ekari kila msimu kwenye udongo. Hii hupanua mavuno kwa 15–30% na iliyobaki hutumiwa na mazao katika msimu ujao.

Kutumia mbolea za kibaiolojia

Ufanisi wa mbolea ya kibaiolojia hutegemea aina ya udongo, hali ya hewa na mbinu za usimamizi wa wadudu na magonjwa. Nyinginezo ni pamoja na mbolea iliyotumika, aina ya viumbe vidogo vilivyotumika, na njia ya matumizi.

Rhizobium hukuzwa kwenye maabara na kuchanganywa na unga wa mkaa. Andaa mchanganyiko, upake kwenye mbegu, kisha eneza mbolea ya kibailojia na uichanganye vizuri. Kaushia mbegu chini ya kivuli na kisha uzipande mapema iwezekanavyo. Azotobacter huongeza mavuno, na vile vile huongeza kilo 10 ya nitrojeni kwenye ekari moja kila msimu, na huboresha uotaji. Azotobacter hutumiwa kutibu mbegu, mizizi na pia huongezwa kwenye udongo moja kwa moja.

Azotobacter pia huchanganywa kwenye mbolea wakati wa kuandaa mbolea. Hutumika kutengeneza vichocheo vya ukuaji wa mimea na kuvihifadhi kwenye udongo, na hivyo kuboresha ukuaji wa mimea. Azobacter huzalisha kemikali ambayo huua viini. Pia huboresha upatikanaji wa fosforasi.

Mbolea nyingine ya kibaiolojia ni azospirillum ambayo pia huongeza nitrojeni ili kuhimiza upatikanaji wa fosforasi, zinki, shaba na salfa. Hii husaidia mimea kunyonya maji na virutubisho na madini. Fosiforasi hupunguka iwapo viwango vya pH vimpenda au kushuka sana. Fosiforasi hupatikana kwa matumizi ya bakteria ambayo huitengeneze (PSB).

Bakteria hii hutumiwa kutibu mbegu, mizizi au huongezwa kwenye udongo moja kwa moja. 200g ya PSB inahitajika kutibu mbegu za ukubwa wa wasitani, na 100g kwa mbegu ndogo. Kwa njia ya kutibu mizizi, changanya kilo 1 ya PSB kwenye lita 10–15 za maji na utumbukize mizizi kwa dakika 5 na kisha upande mapema iwezekanavyo. Kwa njia ya kuongeza shambani moja kwa moja, changanya kilo 3–5 za PSB na kilo 50 za samadi na uongeze. Weka mbolea ya kibaiolojia mahali baridi na epusha mgusano na kemikali yoyote.

Hatimaye, usitumie mbolea ya kibayolojia iliyokwisha muda wake, na tumia aina maalum za rhizobium kwa matokeo mazuri.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:27Mbolea ya kibaiolojia ni mchanganyiko wa viumbe vidogo vinavyotolea mimea virutubisho.
00:2800:38Rhizobium ni mbolea maarufu zaidi ambayo huishi kwenye vinundu vya mimea na huongeza nitrojeni kwenye udongo.
00:3901:18Rhizobium huongeza nitrojeni kwenye udongo na kupanua mavuno kwa 15–30% .
01:1901:28Ufanisi wa mbolea ya kibaiolojia hutegemea aina ya udongo, hali ya hewa na mbinu za usimamizi wa wadudu na magonjwa.
01:2901:40Nyinginezo ni pamoja na mbolea iliyotumika, aina ya viumbe vidogo vilivyotumika, na njia ya matumizi.
01:4101:55Rhizobium hukuzwa kwenye maabara na kuchanganywa na unga wa mkaa.
01:5602:07Andaa mchanganyiko, upake kwenye mbegu, kisha eneza mbolea ya kibailojia na uichanganye vizuri.
02:0802:22Kaushia mbegu chini ya kivuli na kisha uzipande mapema
02:2303:06Azobacter huongeza mavuno na huboresha uotaji.
03:0703:13Azotobacter hutumiwa kutibu mbegu mizizi na pia huongezwa kwenye udongo moja kwa moja.
03:1403:29Azotobacter pia huchanganywa kwenye mbolea wakati wa kuandaa mbolea, hutumika kutengeneza vichocheo vya ukuaji wa mimea na kuvihifadhi kwenye udongo.
03:3003:47Azobacter huzalisha kemikali ambayo huua viini na huboresha upatikanaji wa fosforasi.
03:4804:18Azospirillum kuhimiza upatikanaji wa fosforasi, zinki, shaba na salfa.
04:1904:48Azospirillum husaidia mimea kunyonya maji na virutubisho na madini.
04:4905:21Bakteria hutumiwa kutibu mbegu, mizizi au huongezwa kwenye udongo moja kwa moja
05:2205:43PSB hutumiwa kutibu mbegu, mizizi.
05:4405:55Tumbukiza mizizi kwennye mchanganyiko kwa dakika 5, kisha upande mapema iwezekanavyo.
05:5606:17Weka mbolea ya kibaiolojia mahali baridi na epusha mgusano na kemikali yoyote.
06:1806:32Usitumie mbolea ya kibayolojia iliyokwisha muda wake, na tumia aina maalum za rhizobium
06:3306:50Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *