Wafugaji wa ng‘ombe wa maziwa hutumia teknolojia zilizoboreshwa kwa mfano mfumo wa kukamulia unaojiendesha, ambao ni muhimu sana kwa wakulima na wanyama.
Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa wanapaswa kukamua mara tatu kwa siku kwani huku huongeza uzalishaji wa maziwa na hupunguza mafadhaiko kwa wanyama. Mfumo huo hutambua mabadiliko iwapo kumetokea magonjwa au majeraha.
Faida za mfumo
Mfumo huo huwezesha uzalishaji wa maziwa safi, na hivyo kukidhi mahitaji ya watumiaji.
Pia mfumo huo humwezesha mkulima kutambua ugonjwa wa kiwele, na hivyo kuudhibiti kuenea.
Mfumo huo huhakikisha usafishaji wa maziwa na hivyo basi kuzuia magonjwa.
Mfumo huo vilevile unawezesha kurekodi uzalishaji wa maziwa kwa kutumia kompyuta, na hivyo kuboresha ufugaji wa ng’ombe.
Pia mfumo huo huharakisha ukamuaji wa ng’ombe na vile vile hupunguza matukio ya majeraha kwa matiti.
Wakulima walio na mfumo huo huokoa gharama ya wafanyikazi na pia hugundua kiwango cha uzalishaji wa maziwa kwa kila mnyama.
Mwishowe, mfumo huo husajili historia ya uzalishaji wa mnyama binafsi, na hivyo kumwezesha mfugaji kugundua mabadiliko katika uzalishaji, na hivyo kumshughulikia ifaavyo.