Aina zingine mpya za mpunga hustahimili mafuriko kwa wiki mbili. Ikiwa unaishi katika maeneo yenye mafuriko, uliza muuzaji wako wa karibu mahali unapoweza kupata aina hizi sugu za mpunga.
Pengine, mpunga unaopandwa katika maeneo ya nyanda za chini huharibiwa na mafuriko. Maji ya mafuriko hukaa kwa muda mrefu na hivyo huua mimea, sababu yanazuia muangaza wa jua ambao huhitajiwa na mpunga. Baada ya maji ya mafuriko kupungua, baadhi ya wakulima huendelea kulima mashamba hayo tena. Ila, wanaweza kuwa na changamoto ya kupata miche, mbolea au wasaidi.
Maeneo yenye mafuriko
Ikiwa unaishi katika eneo lenye mafuriko, unafaa kupanda mbegu za aina za mpunga zinazostahimili mafuriko. Hakikisha kwamba mbegu hizo zina afya, na hazijaathiriwa na wadudu au magonjwa. Baada ya kuvuna mpunga, kausha mbegu kwenye jua, kisha zisafishe na kuzihifadhi nyumbani. Kwa hivyo, tumia gunia la polythene ambalo limewekwa ndani ya mfuko wa kitani/ gunia.
Hakikisha kwamba unatumia mbegu thabiti na zenye nguvu. Usipande mbegu nyingi sana, kwa sababu zitakuwa nyembamba na dhaifu na zitaharibiwa na mafuriko kwa urahisi. Ambapo kawaida ungetumia kilo mbili za mbegu, unafaa kupanda nusu kilo tu. Kisha miche itakuwa na nguvu kuishi siku 10 hadi 15 katika mafuriko.
Miche ya wiki nne ina nguvu kuliko miche ya wiki tatu. Kwa hivyo, unafaa kupandikiza zile ambazo ni kubwa kidogo.
Maji ya mafuriko yakipungua, matope yanabaki. Matope haya yanashikilia majani ya mpunga, na huwafanya yashindwe kupumua na kupokea mwangaza wa jua. Kwa hivyo, ni muhimu kuondoa matope haya kwa makini. Hakikisha kuondoa maji yoyote yaliyosalia, magugu au takataka zilizoletwa na maji ya mafuriko.
Usitumie mbolea ya urea moja kwa moja baada ya mafuriko, kwa sababu mimea ya mpunga yataanza kuoza. Wiki moja baada ya maji ya mafuriko kupungua, mimea inaweza kunawiri na kupata virutubisho vipya. Basi hapo unaweza kuongeza kilo 40 za mbolea ya urea kwa hekta, na kilo 40 za mbolea ya potasiamu. Baada ya wiki mbili ongeza tena kilo 40 za urea lakini usiongeze potasiamu tena.