Kuacha nafasi kubwa kati ya mimea ya soya husababisha mavuno machace liche ya juhudu inayofanywa shambani. Mazao yanaweza kuongezeka kwa kutumia msongamano bora wa mimea shambani.
Maharagwe ya soya ni chanzo cha mafuta, protini na madini ambayo ni muhimu kwa afya yetu. Yanaweza kutengenezwa kuwa bidhaa tofauti kama vile; maziwa, unga ulioboreshwa, mafuta ya kupikia na jibini. Kwa kuongeza, mimea ya soya huboresha rutuba ya udongo, na makapi yake ni chanzo cha lishe ya mifugo.
Jinsi ya kupata msongamano bora
Tumia mbegu zinazokua vyema. Mbegu zinafaa kuhifadhiwa kwenye gunia wazi katika mahali ambapo hazigusi ardhi. Maharagwe ya soya yana mafuta mengi, na hivyo hupoteza uwezo wa kuota yakiwa yamehifadhiwa vibaya.
Ili kuhakikisha kama mbegu zitaota vizuri au laa, panda mbegu 100 kwenye chombo au kitalu kidogo na umwagilie maji. Ikiwa baada ya wiki moja angalau mbegu 80 zimeota, basi mbegu hizo ni nzuri.
Kabla ya kupanda mbegu, lima shamba lako tambarare au ukiweka matuta. Usipande kwenye shamba lenye magugu kwasababu mbegu zitakufa. Joto linalotokana kwenye magugu wakati yanaoza huua mbegu. Baada ya kulima, vunja vunja mabonge ya udongo ili kulainisha udongo.
Ni bora kupanda katika mashimo yasiyo na kina kirefu baada ya mvua kubwa. Panda ukiacha umbali mdongo wa 20 cm kati ya miche na 40 cm kati ya safu. Maharagwe ya soya hupokea nitrojeni kutoka hewani na kuitumia kwa kukua, kwa hivyo soya huhitaji virutubisho vichache kutoka kwenye udongo.
Mara tu baada ya kupanda, dhibiti viumbe vamizi haswa ndege. Panda mbegu nne kwa kila shimo kwasababu zingine zinaweza kuharibiwa, na pia punguza miche na ubakishe miwili kwa shimo wakati wakupalilia.
Baada ya wiki chache, sungura wa porini watakuwa tishio tu lakini wadhibiti kwa kuwawinda usiku na kuweka mitego shamba.