Parachichi ni chakula muhimu chenye virutubisho kwa wakulima na walaji kwa ajili ya chakula na mapato. Kupanda mmea wa parachichi ni rahisi na inahitaji hatua rahisi na ujuzi.
Hatua za kupanda
Chagua eneo lisilo la maji mengi, na udongo tifutifu au udongo wa mfinyanzi ambao husababisha mizizi kupenyeza vyema bila kuoza.
Pili, chimba mashimo ya kina cha futi 2 na upana wa futi 2 kwa ukuaji sahihi wa mizizi ya mmea.
Andaa nyenzo zitakazotumika kupanda kama vile samadi iliyooza, na mbolea ya madini ambayo huhimiza ukuaji wa mizizi.
Changanya mbolea na udongo, na uweke mchanganyiko kiasi ndani ya shimo.
Panda mche na ujaze udongo hadi kufikia kiwango ambapo miche iliunganishwa au kufikia kiwango cha udongo wa kitalu.
Himiza mche kusimama wima na mwagilia maji tu bada ya kupanda ili kuepusha mmea kunyauka na kukauka.