»Ndani ya Kakuzi: Uzalishaji Bora wa Makadamia (Karanga pori)«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=KuL_j1xrCto&t=354s

Muda: 

00:07:41
Imetengenezwa ndani: 
2020

Imetayarishwa na: 

Kakuzi Plc

Makadamia au karanga pori ni zao muhimu kwa ajili ya mafuta yake yenye faida ambayo husaidia kuimarisha afya zetu.

Uzalishaji na usindikaji

Anzia kwenye kitalu kwa kuchagua aina za mbegu zinazohitajika na uzipandikize ili kutoa miche bora. Panda miche kwenye udongo usio na maji mengi, kwenye mteremko kwa muachano sahihi.

Baada ya kupanda, tunze miti kwa kuweka mbolea, kupalilia na kumwagilia maji katika nyakati za awali. Baada ya kuanzishwa, makadamia hustahimili hali ya ukame lakini unaweza kumwagilia maji ili kudumisha kiwango cha uzalishaji na ubora wa juu.

Mti wa makadamia unaotunzwa vizuri huanza kutoa karanga wakati miaka 4, lakini mavuno mazuri huanza baada ya mwaka wa 5. Fanya vipimo vya ukomavu kabla ya kuvuna. Wakati wa kuvuna, weka karanga kwenye mifuko safi. Pima uzani wa karanga, na kisha pakia mifuko kwenye matrela safi na kusafirishwa kiwandani.

Zikifika kiwandani, karanga hukatwa maganda, na kukaushwa hadi kufikia kiwango cha unyevu wa 10%. Kisha karanga hupelekwa kwenye kituo cha kupasuliwa ambapo unyevu hupunguzwa zaidi hadi 1.5% kabla ya kupasuliwa. Baadaye, bidhaa hiyo hupakiwa na ni tayari kuuzwa nje.

Kutoka kwa usindikaji wa makadamia, tunapata maganda ambayo yanaweza kuoza kuwa mbolea na kurudishwa shambani. Maganda pia yanaweza kutumika kama kuni.

 

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:29Makadamia au karanga pori ni zao muhimu kwa ajili ya mafuta
00:3001:39Anzia kwenye kitalu kwa kuchagua aina za mbegu na uzipandikize.
01:4002:38Baada ya kupanda, weka mbolea, palilia na mwagilia maji
02:3903:30Mavuno huanza baada ya miaka 4. Fanya vipimo vya ukomavu kabla ya kuvuna.
03:3103:48Wakati wa kuvuna, weka karanga kwenye mifuko safi. Pima uzani wa karanga, na safirisha kiwandani.
03:4904:28Karanga hukatwa maganda, na kukaushwa na kupasuliwa kiwandani.
04:2904:47Baada ya kupasuliwa, bidhaa hupakiwa na ni tayari kuuzwa nje
04:4805:36mabaki na maganda ya makademia yanaweza kusindikwa kuwa mbolea na kuni.
05:3706:27Dumisha afya ya wafanyikazi na usafi.
06:2807:41Dumisha ubora wa mazao.

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *