Quinoa ni bidhaa inayohitajika sana, lakini viwavi hufanya upandaji wake kuwa mgumu. Nyigu husaidia kuharibu viwavi na kwa hivyo, kuwezesha kupata mavuno bora.
Wakulima wengi nchini Bolivia wameanza kupanda mashamba makubwa ya quinoa kwa mara ya kwanza, kwa sababu quinoa ni bidhaa maarufu na inayohitajiwa. Lakini tangu mimea ilipoharibiwa, viwavi wanaokula majani na nafaka za quinoa wamegeuka shida kubwa.
Nyigu anayechimba
Baadhi ya nyigu wakubwa huwinda viwavi. Nyigu anayechimba huonekana wakati wa masika na kiangazi. Nyigu huo hula nekta/majimaji ya maua, na maua ya mwituni kama vichaka au nyasi. Viota vyao vina urefu wa 3 cm hadi 7 cm kwenye udongo. Nyigu huwalisha watoto wao viwavi.
Nyigu hudunga kiwavi na kuweka sumu ambayo kumlalisha kiwavi. Kisha, nyugi huleta kiwavi kwenye kiota chake. Katika kiota, nyugi hutaga yai moja kwenye mwili wa kiwavi. Kisha, nyigu hufunga kiota na mchanga ili mdudu mwingine asiingie.
Katika kiota, funza mdogo huanguliwa na kula kiwavi. Kisha funza hujenga kifukofuko na kulala wakati wa majira ya baridi.
Katika wakati wa masika na kiangazi, nyigu zaidi hutoka kwenye vifukofuko vyao na kuanza duru ya maisha tena. Kwaani, nyigu huwinda viwavi kila wakati, na kwa hivyo kulinda mimea ya quinoa, kwa sababu viwavi ndio wadudu amabao huvamia quinoa.
Vidudu vyenye faida.
Badala ya kutumia dawa za kuua wadudu, tunza nyigu na wadudu wengine wazuri. Nyigu huhitaji maua kabla ya kutaga mayai, ili wafyonze umajimaji mtamu (nekta). Kwa hivyo, unafaa kupanda mimea ya asili ili kuwapa chanzo kizuri cha chakula na makao. Na pia, unalinda udongo dhidi ya upepo na mmomomyoko.