Udongo ukitunzwa au kuhifadhiwa, waweza kupanda mazao ya pili kama mahindi na ngano wakati wa kiangazi. Unaweza kutumia njia mbili: kulima kwa mistari na kupanda kitalu
Udongo hukaa unyevu kwa mda mrefu unapoacha mabaki ya mimea shambani. Lakini wakulima wengi hulima mashamba yao kabla ya kupanda na hawaachi mabaki ya mimea. Kwa hivyo udongo hupoteza rutba na kukauka haraka.
Zao la pili
Wakulima nchini Bangladesh hupenda kutumia mitambo au mashine ambazo hupanda mazao mapema bila kulima shamba lote. Kwa hivyo wanaweza kupanda mazao bora wakati wa kiangazi. Wanavuna zaidi na kuokoa wakati, maji na pesa
Kilimo cha ukanda
kwa aina mbalimbali za mpunga, una uwezo wa kupanda zao la msimu wa kiangazi mapema. Unaweza kuanza kupanda mahindi na ngano wiki moja mapema. Kwa hivyo, haulimi shamba lote baada ya kuvuna mpunga. Trekta ya magurudumu mawili ilio na sanduku maalum inaweza kupanda mbegu na kusambaza mbolea.
Unapoondoa baadhi ya jembe ukalima mstari mwembamba wa ardhi , utaona kwamba mabua hubaki. Udongo uliobaki huendelea kukaa imara na mazao ya pili yanaweza kukua vizuri. visu vinafaa kukata mpunga kwa takribani sentimita 30 juu ya ardhi, ili mabaki wa mimea yatoe unyevu wa udongo kwa muda mrefu.
Kulima ukanda huokoa maji, kazi na mafuta kwa hivyo wakulima na watoa huduma hufaidi.
Kupanda kitalu
Njia nyingine ya kuokoa maji, kazi na pesa ni kupanda kitalu. Kwa hivyo, kuna jembe zinazozunguka ambazo hulima udongo. Udongo huunda maumbo yanayofanana na vitalu.
Ukipanda mimea yako kwenye vitalu ni rahisi kumwagilia, kuokoa maji, na kudhibiti panya. Vitalu husababisha upenyezi wa mwangaza wa jua kupitia, ambayo panya hawapendi, na kumwagilia hufanya udongo kuwa thabiti kwenye mifereji, kwa hivyo panya hukaa huko chini.
Mashine ya upandaji wa kitalu husambaza mbolea, pamoja na kupanda mbegu, kama vile trekta ya kulima.