Ufugaji wa kuku ni biashara yenye faida kubwa ambayo hutoa mapato kwa muda mfupi kwa gharama nafuu.
Kabla ya kuanza biashara ya ufugaji kuku, fanya utafiti kuhusu mitaji, kanuni za ufugaji, na mbinu za usimamizi ili kuepuka hasara. Kwa kawaida ni vyema kuanza kidogo kidogo na kuwekeza tena ili kupanua biashara. Aina tofauti za kuku zina nyakati tofauti za kurudisha faida, kwa mfano kuku wanaozalisha mayai hutoa faida baada ya siku 30 huku kuku wa nyama wakitoa faida kati ya wiki 6–8.
Faida za kuku
Kuku hutoa faida ya haraka, na ni rahisi kufanya makadirio ya mapato.
Kuku huhakikisha mapato endelevu kwa mfano kupitia kuuza mayai na ndege
Bidhaa za kuku huhitajika sana katika masoko ya ndani na nje ya nchi, na huleta mapato zaidi kwa wafugaji.
Mapato kutoka kwa ndege yanaweza kutumika kuwekeza katika biashara zingine, na hivyo kuwaongezea kipato wafugaji.
Wafugaji wa kuku hupata kutambuliwa katika jamii kwa sababu wakati mwingine hutoa ndege kwa maskini kwa mfano wakati wa misimu ya sikukuu.
Mashamba ya kuku yanaweza kufuatiliwa kwa urahisi kutoka mbali, hii huwapa wafugaji muda wa kufanya shughuli nyingine za biashara.
Kuku huhitaji gharama nafuu ya kazi, utunzaji mdogo na wafanyakazi wenye ujuzi mdogo, hivyo faida kubwa hupatikana.