»Shamba la mbuzi – Jinsi ya kuanzisha ufugaji wa mbuzi kwa uwekezaji mdogo «

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=lrVxHATPkQM

Muda: 

00:04:31
Imetengenezwa ndani: 
2021

Imetayarishwa na: 

Business Ideas English

Kwa kuwa ni biashara yenye faida kubwa, ubora na wingi wa bidhaa zinazopatikana kwa ufugaji wa mbuzi aina ya bangal hubainishwa na mbinu ya uzalishaji inayotumika.

Mbuzi aina ya bengal hutoka nchini Bangladesh na ufugaji wao ni biashara yenye faida kubwa. Mbuzi hawa ni chanzo kizuri cha nyama, na pia huzaa watoto wengi, yaani mara mbili kwa mwaka.

Usimamizi wa mbuzi

Mbuzi aina ya bengal hustahimili hali ya hewa yoyote, na hivyo hufugwa sana. Ufugaji wa mbuzi ni chanzo kizuri cha kipato, ajira na huhitaji kibarua kidogo kwani mbuzi wa hawa wama mwili mdogo, na hivyo huhitaji makazi kidogo.

Vile vile, nafasi ya takriban futi 10 za mraba inahitajika kwa kila mbuzi. Kwa mbinu ya banda lililoinuliwa, unahitiaji futi 20–25 za mraba kwa kila mbuzi. Hakikisha kuna uingizaji mzuri wa hewa ndani ya banda, na pia jenga uzio kuzunguka banda ili kuwalinda mbuzi dhidi ya wanyama wawindaji. Hifadhi vyombo vyote vya kulishia na kunyweshea maji ndani ya chumba. Tengeneza vyumba tofauti ili kutenganisha mbuzi wa kuzaliana, wajawazito na wanaonyonyesha.

Banda lazima liwe na sakafu ya mbao, na liinuliwe kwa urefu wa futi 4–5 kutoka ardhini, na futi 6–8 kutoka kwa sakafu hadi paa. Sakafu lazima iwe na miachano kati ya mbao ili mkojo wa mbuzi utiririke chini kwa urahisi. Weka damani za plastiki kwenye madirisha ili kuwalinda mbuzi dhidi ya baridi kali. Weka mbuzi aliezaa na watoto katika sehemu maalum usiku katika wakati wa msimu wa kibaridi.

Safisha banda kila asubuhi. Tolea mbuzi lishe bora kwa ukuaji bora. Watolee maji safi, tunza dume bora kwa ajili ya kuzaliana kiasili. Tenganisha mbuzi wajawazito kabla ya kuzaa.

Watoto wanapaswa kuzaliwa katika sehemu kavu, na lazima wasafishwe baada ya kuzaliwa. Mpe mtoto maziwa ya kwanza saa chache baada ya kuzaliwa ili kuongeza kingamwili. Walishe watoto kwa kutumia njia bandia wakati maziwa ya mama hayatoshi.

Hatimaye, chanja mbuzi na uwe na uhusiano mzuri na daktari wa mifugo.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:14Ufugaji wa mbuzi aina ya bengal ni biashara yenye faida kubwa.
00:1500:45Mbuzi hawa ni chanzo kizuri cha nyama, na pia huzaa watoto wengi
00:4600:54Hustahimili hali ya hewa yoyote
00:5501:04Hufugwa ka wingi, na kwa uchache.
01:0501:20Ufugaji wa mbuzi ni chanzo kizuri cha kipato, ajira na huhitaji kibarua kidogo.
01:2101:39Mbuzi wa hawa wama mwili mdogo, na hivyo huhitaji makazi kidogo
01:4001:51Nafasi ya takriban futi 10 za mraba inahitajika kwa kila mbuzi.
01:5201:59Hakikisha kuna uingizaji mzuri wa hewa ndani ya banda, na pia jenga uzio kuzunguka banda.
02:0002:03Hifadhi vyombo vyote vya kulishia na kunyweshea maji ndani ya chumba
02:0402:08Tengeneza vyumba tofauti ili kutenganisha mbuzi wa kuzaliana, wajawazito na wanaonyonyesha.
02:0902:18Banda lazima liwe na sakafu ya mbao, na liinuliwe kwa urefu wa futi 4–5 kutoka ardhini, na futi 6–8 kutoka kwa sakafu hadi paa.
02:1902:38Sakafu lazima iwe na miachano kati ya mbao. Weka damani za plastiki kwenye madirisha.
02:3902:42Weka mbuzi aliezaa na watoto katika sehemu maalum usiku katika wakati wa msimu wa kibaridi.
02:4302:51Safisha banda kila asubuhi.
02:5203:21Tolea mbuzi lishe bora kwa ukuaji bora.
03:2203:30Watolee maji safi
03:3103:51Tunza dume bora kwa ajili ya kuzaliana kiasili. Tenganisha mbuzi wajawazito kabla ya kuzaa.
03:5204:03Watoto wanapaswa kuzaliwa katika sehemu kavu, na lazima wasafishwe baada ya kuzaliwa.
04:0404:18Mpe mtoto maziwa ya kwanza saa chache baada ya kuzaliwa.
04:1904:24Walishe watoto kwa kutumia njia bandia wakati maziwa ya mama hayatoshi.
04:2504:29Chanja mbuzi na uwe na uhusiano mzuri na daktari wa mifugo.
04:3004:41Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *