Kwa kawaida ng’ombe huzaa baada ya miezi 9 ya ujauzito. Hata hivyo, kuna taratibu kadhaa zinazopaswa kutekelezwa na kuzingatiwa na wafugaji wakati wa kuzaa ndama.
Kwa hiyo, ni muhimu kuwahamisha ng‘ombe wajawazito kwenye zizi lisilo na utelezi wiki 2 kabla ya kuzaa. Zizi linapaswa kusafishwa na kuuliwa viini vinavyosababisha magonjwa. Inashauriwa pia kutosumbua ng‘ombe anayezaa isipokuwa usaidizi unahitajika kwani huku kunanaweza kuzuia uwezo wa mnyama kuzaa vizuri.
Hatua zinazohitajika
Baada ya kuzaa, ruhusu mama kumramba ndama aliyezaliwa ili kuboresha mzunguko wa damu.
Pia ondoa kamasi puani na masikioni mara moja ili kuzuia kuziba na kuwezesha ndama kupumua. Safisha ndama aliyezaliwa kwa kitambaa safi na mabua ya mpunga yaliyokatwakatwa ili kumkausha ndama.
Funga kitovu 2.5cm kutoka kwa mwili wake na kata kitovu 1cm chini ya mfungo. Kisha chovya sehemu ya kitovu iliyokatwa kwenye mmumunyo
wa viuavijasumu ili kudhibiti maambukizi.
Mpime ndama aliyezaliwa ili kutambua uzani wake, na kumpa ndama maziwa ya kwanza ndani ya saa 1 baada ya kuzaliwa. Maziwa ya kwanza kutoa virutubisho na kingamwili kwa ndama mchanga.
Tenganisha ndama wachanga kutoka kwa mama na uwatolee huduma ya kutosha ili kuzuia vifo vya ndama.
Uwapo kuna changamoto katika kuzaa, mpe mnyama usaidizi ufaao. Hatimaye, ondoa kondo la nyuma linaposhindwa kushuka kiasili ndani ya saa 8.