Demi-lunes au kingamaji za nusu duara ni rahisi kutengeneza, na ni mbinu bora ya kuvuna maji katika Afrika Magharibi tangu 1980.
Mbinu hii ilikuwa rahisi kueleweka, wakulima waliiona kuwa bora kwa kuwa iliwawezesha kufanya kazi kwa vikundi. Mstari wa kontua hutengenezwa kwanza kwa kutumia kifaa maalum, A-fremu huzungushwa kando ya mstari wa kontua ili kuchora nusu duara kwa kutumia ncha zake. Udongo hulimwa na mbolea kuongezwa ili kurutubisha ardhi.
Kupanda mbegu
Mbegu za nyasi hupandwa ili mvua inaponyesha, maji huelekezwa kwenye demi-lunes, kisha hupenyeza kwenye udongo na hivyo kuboresha hali ya udongo ambayo hustawisha ukuaji wa nyasi. Miche hushughulikiwa na watumiaji wa ardhi. Changamoto kubwa zinazowakabili wakulima ni upatikanaji wa mbolea za madini zitakazotumika katika demilunes.
Jamii nyingi za viumbe hai
Demilunes zina matumizi mengi. Huhimiza uotaji wa mbegu na ukuzaji wa aina za miti ya kienyeji. Pia ni rahisi kutengeneza na ni bei nafuu. Zinaweza kutumika katika kilimo cha mimea, nyasi au miti, na zimekuwa teknolojia endelevu ya uvunaji wa maji katika eneo la Sahel.
Uvunaji wa maji kupitia mbinu ya demilunes husaidia kurejesha jamii nyingi za viumbe hai katika maeneo ambayo mimea imeathiriwa na ukame. Hii ina manufaa makubwa kwa watu na wanyama katika uzalishaji wa chakula.