Soya ni zao muhimu kwa wakulima, wafanyabiashara na walaji kwani ni chanzo cha mapato, chakula na pia huongeza nitrojeni kwenye udongo.
Kukuza zao la aina hiyo kunahitaji mbinu fupi fupi rahisi, na hivyo kuboresha ugavi wa chakula. Hata hivyo, kabla ya kujihusisha na shughuli hizi zote unapaswa kuanza mchakato kwa kupata aina nzuri za mbegu zilizoidhinishwa kutoka vyanzo vya uhakika.
Hatua za kilimo
Kwanza andaa ardhi kwa kufyeka na choma takataka nzito. Kwa kilimo maalum, nyunyizia ardhi kemikali za kuua magugu na kisha lima ardhi ili kulainisha udongo. Panda kwa muachano wa sm 5-10 ndani ya safu, na muachano wa sm 60 kati ya safu. Panda kwenye mashimo ya kina cha sm 1-2 baada ya mvua kunyesha vizuri. Panda mbegu 1-2 na kisha kufunika mbegu kwa udongo laini.
Hakikisha unadhibiti magugu kila wakati hasa kati ya siku ya 5 nhadi 35 baada ya kupanda ili kupunguza ushindani wa virutubisho. Vuna majani ya mmea yanapogeuka manjano, kusanya mimea kwenye sehemu moja ili kurahisisha ukusanyaji wa maharage yanapodondoka kutoka kwenye maganda wakati wa kupura.