»Tunda la mpera«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.youtube.com/watch?v=BtxtEw_YJYY

Muda: 

00:04:37
Imetengenezwa ndani: 
2018

Imetayarishwa na: 

Business Ideas English.

Mapera hutamaniwa sana kutokana na faida zao za kiafya. Kujifunza jinsi ya kupanda tunda hili huwasaidia wakulima kuongeza kipato chao.

Hata hivyo, tunda hili lina wadudu waharibifu wengi, ambao ni pamoja na nzi wa matunda, vidukari sufu, vipekecha, viwavi, nzi mweupe, nakadhalika. Mipera iliyobebeshwa hukomaa haraka katika miaka 2 hadi 3 ikilinganishwa na mbegu ambazo kuchukua miaka 4 hadi 5.

Zana zinazofaa zinazotumika kuvuna mapera ni visu au mashine za kung‘oa matunda.

Kupanda hadi kuvuna

Kabla ya kupanda, inua ardhi na upande katika mfumo wa upandaji wa pembe sita. Panda mche katika shimo la mita za ujazo 0.75 hadi 1 ili kuzuia maji kutwama, na kusababisha ukuaji bora wa mmea. Panda kwenye mashimo ya sm 60 kwa 60 kutegemea na usambazaji wa mvua, kwa umbali wa mita 5–6 katika majira ya kiangazi. Jaza mashimo na kilo 20–25 za samadi ya mifugo, gramu 500 za mbolea ya SSP, gramu 50 za unga wa linden na 1 kg ya majani ya mwarobaini ili kudhibiti mchwa kwa kusababisha ukuaji bora.

Ili kukuza mimea mizuri unapaswa kupanda mimea kutoka kwa vyanzo vilivyoboreshwa. Nyunyiza miti na kilo 0.45 ya salfa ya zinki, na kilo 0.34 ya chokaa iliyoyeyushwa katika lita 70 hadi 74 za maji ili kuongeza virutubisho vya zinki. Hata hivyo, kabla ya kuchana maua, nyunyiza asilimia 0.4% ya asidi ya boroni, na 0.3% ya salfa ya zinki au 0.2% hadi 0.4% salfa ya shaba ili kuongeza mavuno na ukubwa wa matunda.

Dhibiti magugu ili kuhakikisha ukuaji wa mimea yenye afya, punguza ushindani wa virutubisho na pia simamisha mimea kwa vijiti ili kuepuka mashina dhaifu. Vuna matunda kwa mikono ili kuhimiza ukuaji wa matawi ya pili. Nyunyizia dawa zinazopendekezwa kudhibiti wadudu waharibifu wa mapera. Vuna ukitumia zana zinazofaa kwatika wakati sahihi. Jua kwamba mimea iliyobebeshwa hukua haraka.

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0000:35Mapera ni chanzo cha mapato, yanahitaji ardhi ndogo, pembejeo ndogo na hutoa mavuno mengi.
00:3600:00Mipera hustawi katika hali ya umwagiliaji na mvua, na aina zote za udongo.
00:0001:18Mapera yanahitaji kiasi kikubwa cha mboji, pH ya udongo ya 4.5 hadi 8.2, joto la 23 hadi 28 digrii centigrade, na mvua wa 150 cm kila mwaka.
01:1901:34Inua ardhi na panda katika mfumo wa upandaji wa pembe sita kwenye shimo la mita za ujazo 0.75 hadi 1.
01:3501:50Panda kwenye mashimo ya sm 60 kwa 60 kutegemea na usambazaji wa mvua kwa umbali wa mita 5–6 katika majira ya kiangazi
01:5102:01Jaza mashimo na kilo 20–25 za samadi ya mifugo, gramu 500 za mbolea ya SSP, gramu 50 za unga wa linden na 1 kg ya majani ya mwarobaini
02:0202:20Panda mimea kutoka kwa vyanzo asili vilivyoboreshwa. Mwagilia maji
02:2102:39Nyunyiza miti na kilo 0.45 ya salfa ya zinki, na kilo 0.34 ya chokaa iliyoyeyushwa katika lita 70 hadi 74 za maji.
02:4002:56Wakati wa kuchana maua, nyunyiza asilimia 0.4% ya asidi ya boroni, na 0.3% ya salfa ya zinki au 0.2% hadi 0.4% salfa ya shaba.
02:5703:37Dhibiti magugu, punguza ushindani wa virutubishi na pia simamisha mimea kwa vijiti. Pogoa mmea
03:3804:11Nyunyizia dawa zinazopendekezwa kudhibiti wadudu waharibifu wa mapera
04:1204:37Vuna ukitumia zana zinazofaa kwatika wakati sahihi

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *