»Tuzalishe mahindi zaidi«

0 / 5. 0

Chanzo:

https://www.accessagriculture.org/lets-produce-more-maize

Muda: 

00:09:09
Imetengenezwa ndani: 
2016

Imetayarishwa na: 

Tv-Agro-CentroAmerica

Kwa kutumia mbolea kwenye shamba la mahindi, unaweza kupata matokeo bora ya mavuno.

Ikiwa mavuno yako ya mahindi ni kidogo, unaweza kutumia mbolea kuyazidisha. Kwa kutumia mbolea, lazima upande mbegu kidogo kwa tuta kuyafanya matuta yakaribiane. Kwa hivyo, mimea hutumia vizuri; mbolea, maji na muangaza wa jua. Udongo ambao hauna mbolea ya kikaboni nyingi hupoteza rutuba.

Kupanua uzalishaji

Tafuta aina nzuri ya mbegu ambayo kwamba huzaa sana, huchipuka vizuri na pia huzoea asili, kama vile hali ya hewa na ardhi. Aina zingine za mahindi zinaweza kuhifadhiwa shambani, halafu zingine zinafaa kununuliwa kila mwaka. Unafaa kupanda mahindi sentimita 80 kati ya mtaro na sentimita 40 kati ya matuta. Panda mbegu mbili kwa kila tuta. Ongeza kikaboni kama vile mbolea, samadi ya kuku, mabaki ya mimea, maganda ya kahawa kwenye udongo. Ikiwa una uwezo, basi fanya uchambuzi wa udongo. Tumia mbolea siku nane baada ya kupanda. Kwa muda wa siku tano, miche za mahindi hutoka ardhini na zina majani matatu. Kulingana na mwangaza wa jua na bajeti yako, unaweza kuweka hadi mifuko minne ya mbolea ya misombo kwa hekta. Mbolea huzikwa kama vile na mahindi. Kwa hivyo upepo na mvua huwezi kuichukua. Weka mbolea sentimita 5 mbali na mahindi ili kuepuka kuathiri mizizi. Ikiwa una mteremko, zika mbolea upande wa juu ili iweze kuteremka. Mbolea ya msombo inafaa kuwekwa tena siku 25 baada ya mahindi kutoka. Hii husaidia mimea kuwa na chakula kingi wakati inakua. Panda mbegu mbili kwa kila tuta. Ongeza kikaboni kama vile mbolea, samadi ya kuku, mabaki ya mimea, maganda ya kahawa kwenye udongo

Kuanzia dakika ya Hadi dakika y Maelezo
00:0001:03Chukua aina nzuri ya mbegu
01:0401:53Panda mahindi sentimita 80 kati ya mtaro na sentimita 40 kati ya matuta.
01:5402:16Panda mbegu mbili kwa kila tuta kwa umbali udogo, ili mimea yapate virutubisho,maji na mwangaza wa jua.
02:1703:28Changanya mbolea ya kikaboni pamoja na mbolea ya madani
03:2903:54Weka mbolea wakati mmea ukitoa majani matatu
03:5504:08Weka mbolea sentimita 5 mbali na mahindi ili kuepuka kuathiri mizizi.
04:0904:42Unaweza kuweka hadi mifuko minne ya mbolea ya misombo kwa hekta
04:4305:10Ongeza kikaboni kama vile mbolea, samadi ya kuku, mabaki ya mimea, maganda ya kahawa kwenye udongo
05:1106:12Weka mbolea sentimita 5 mbali na mahindi
06:1306:57Zika mbolea ili isichukuliwe na upepo, na mvua.
06:5807:19Hatua tatu za kuweka mbolea: Baada ya siku 8, baada ya siku 25, baada ya siku 40 weka urea.
07:2009:09Muhtasari

Tazama video ya nje

Kwa kubofya kiunga kifuatacho au kitufe cha kucheza utaondoka kwenye Maktaba ya Video ya FO na utumie tovuti ya nje! Tungependa kukuona tena, kwa hivyo usisahau kurudi!

Soma zaidi

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *