Wanyama waharibifu husababisha uharibifu wa mimea, na kupunguza sana mavuno. Wanyama hula majani ya mimea, na pia husababisha uotaji duni pamoja na kuharibu mmea kabisa.
Hata hivyo, kufuata miongozo ifaayo ya udhibiti wa wadudu hupunguza uharibifu unaosababishwa na wadudu kwa kuongeza mavuno ya mimea kama vile kunde, soya na karanga.
Udhibiti wa wadudu
Tibu na chanja mbegu kabla ya kupanda, lakini kufanya huku ni bora baada ya kushauriana na mshauri.
Ili kudhibiti panya, weka mitego au chambo zenye sumu kuzunguka shamba.
Dhibiti wadudu kwa kupanda aina sugu za mbegu.
Tumia dawa za kemikali iwapo uvamizi wa wadudu ni mkubwa na unaweza kusababisha hasara ya kiuchumi.
Kwa udhibiti wa minyoo fundu, tumia mzunguko wa mazao na kanuni sahihi za usafi wa shamba.
Hatimaye, dhibiti magugu shambani kwa sababu haya yanaweza kuhifadhi wadudu waharibifu.