Mbinu mbalimbali za kudhibiti na kuzuia viwavijeshi katika mahindi zimepanua uzalishaji. Hata hivyo, ufanisi wa mbinu hizo hutofautiana, na hivyo gharama ya uzalishaji huongezeka.
Mahindi huathiriwa na viwavijeshi katika hatua zote za ukuaji, na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa wa mazao.
Muda wa maisha ya viwavijeshi ni siku 32 hadi 46 kulingana na halijoto iliyopo.
Halijoto la juu huongeza idadi ya viwavijeshi.
Mzunguko wa maisha
Mayai huanguliwa kwa muda wa siku 2 hadi 4 na kuwa mabuu (viwavi), ambao hula majani kwa muda wa siku 15 hadi 28.
Kiwavi huanguka chini na kuingia ardhini 2cm hadi 3, na baadaye hugeuka kuwa kifukofuko. Baada ya siku 7 hadi 14, nondo mpya huibuka.
Nondo wa kike hufa mara baada ya kutaga mayai, na nondo wazima huhamia umbali wa 100 km kupitia upepo.
Viwavi vilivyoanguliwa hukaa kwenye makutano kati ya shina na majani, ambapo huwa wanakula na kutoboa mashimo, na baadaye huenea kwa mimea mipya.
Viwavijeshi huathiri hadi 80% ya mazao iwapo havijadhibitiwa vizuri.
Athari ya udhibiti wa kemikali
Kemikali husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Kemikali huua viumbe hai muhimu, na pia huathiri afya ya watu, pamoja na kuongeza uvumilivu kwa wadudu hatari.
Udhibiti wa kibiolojia
Udhibiti jumuishi wa wadudu unahusisha matumizi ya wadudu asili ambao hula na kuharibu viwavijeshi, na hivyo kudhibiti wadudu waharibifu shambani na kupunguza matumizi ya viuatilifu.
Mifumo ya udhibiti wa kibiolojia ni pamoja na udhibiti kupitia wadudu asili ambao hula wadudu waharibifu.