Viazi ni mojawapo ya mazao muhimu ya chakula na biashara katika Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, lakini hukabiliwa na changamoto nyingi. Mnyauko wa bakteria wa viazi ni changamoto kubwa.
Mavuno ya viazi barani Afrika ni kidogo kwa sababu ya magonjwa, ukosefu wa mbegu safi, rutuba duni ya udongo, afya duni ya udongo na usimamizi duni wa mazao. Nchini Uganda, Kenya na Ethiopia, mavuno yanayoweza kufikiwa ni takiribani tani 10 kwa hekta, wakati mavuno yanayoweza kupatikana ni kati ya tani 30 hadi 35 kwa hekta. Ugonjwa huenea kupitia udongo na mbegu zilizoathirika. Barani Afrika, hali inazidishwa na ukosefu wa ujuzi wa wakulima kuhusu masuala muhimu ya afya na usimamizi wa udongo.
Biolojia ya ugonjwa
Katika shamba, ugonjwa huo hutambuliwa kwa mchakato unaoitwa bacterial ooze test ambapo shina la mmea unaonyauka hukatwa na kuning’inizwa kwenye glasi yenye maji safi, na endapo mmea huo umeambukizwa, majimaji ya bakteria huonekana yakitoka nje mwa shina.
Mnyauko bakteria ni ugonjwa unaoenezwa na mbegu na udongo, na hustawi shambani kwa muda mrefu shambani iwapo kuna mmea wa kuuendeleza. Ugonjwa huo huenea sana katika viazi na mazao ya jamii hiyo hiyo.
Ugonjwa huu pia unaweza kustawi kwenye mmea bila kuonesha dalili zozote, na hivyo unaweza kusitotambuliwa kwa urahisi na macho. Kadhalika, ugonjwa unaweza kuenea kwenye maeneo mengine kupitia njia ya mbegu, na hivyo utunzaji unapaswa kuchukuliwa.
Udhibiti wa mnyauko
Utafiti umefanywa ili kuanzisha wakala za udhibiti wa kibaiolojia ambazo husaidia kukandamiza mnyauko wa bakteria. Wakala tano za udhibiti wa kibaiolojia zimepatikana kukandamiza mnyauko bakteria hadi 80%. Hizi hutumiwa pamoja na hatua zingine za udhibiti.
Katika udhibiti wa mnyauko, zingatia masuala makuu matatu; Kutayarisha mpango wa mzunguko wa mazao ili kudhibiti ugonjwa huo, kuboresha rutuba ya udongo na kutumia nyenzo safi za upandaji.